KAGERA WAZITAKA POINTI ZAO ZIRUDISHWE, WATUMA BARUA TFF - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Saturday, April 15, 2017

KAGERA WAZITAKA POINTI ZAO ZIRUDISHWE, WATUMA BARUA TFF

KLABU ya Soka ya Kagera imeiandikia barua Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) kulalamikia maamuzi yaliyotolewa na kamati ya saa 72 kwa kuipatia pointi tatu timu ya Simba ikidaiwa wamemchezesha mchezaji mwenye kadi tatu za njano.

Barua hiyo iliyopelekwa moja kwa moja kwa Mtendaji Mkuu wa TFF, Selestine Mwesigwa imeandikwa na Mwenyekiti wa klabu hiyo  Hamis Mdaki na kuelekeza malalamiko yao ya kutokubaliana na maamuzi ya kamati ya saa 72.

Hukumu ya kuipatia Simba alama hizo ilitoka juzi usiku baada ya Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Mohamed Yahya  alitoa maamuzii hayo mbele ya waandishi wa habari na kusema kuwa kamati imethibitisha kuwa Mchezaji Mohamed Fakhi alikuwa na kadi tatu za njano alizozipata katika michezo dhidi ya Prisons, Majimaji na African Lyon.

Hukumu hiyo imeonekana kutokukubalika kwani kamati ilishindwa kupitia ripoti za waamuzi baada ya kuonekana kutofautiana baina ya mwamuzi na kamisaa wa mchezo na kuamua kuwaita waamuzi waje kuthibitisha kama ni kweli Fakhi alipewa kadi ya njano.

Kagera wamemtaka katibu mkuu kuiangalia upya hukumu hiyo kwani wana uhakika kuwa Fakhi alikuwa na kadi mbili za njano na sio tatu kama wanazodai Simba. Katika mchezo huo wa Kagera walifanikiwa kutoka na ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Simba uliochezwa kwenye dimba la Uwanja wa Kaitaba Mkoani Kagera.


Baaada ya maamuzi hayo Simba wamejikita kileleni zaidi wakiwa na alama 61 wakifuatiwa na Yanga wenye alama 56.


No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages