Meneja Mwandamizi Kitengo
cha Amana, Bima na Huduma za ziada wa Benki ya NMB, Bw. Stephen Adili (kushoto)
akitoa maelezo namna benki hiyo inavyowakumbuka vijana katika bidhaa zao
mbalimbali kwa wageni waalikwa, Mkurungenzi Mkuu wa UN CDF Tanzania, Peter
Malika (wa kwanza kulia) na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa
Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (wa pili kulia)
walipotembelea banda hilo kwenye uzinduzi wa mjadala kujadili changamoto
mbalimbali na kuhamasisha vijana nchini kupata uelewa wa masuala ya fedha.
Meneja Mwandamizi Kitengo cha Amana, Bima na Huduma za ziada wa Benki ya NMB, Bw. Stephen Adili (kulia) akizungumza na vijana katika kampeni zilizowakutanisha vijana na kujadili changamoto mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kuhamasisha vijana nchini kupata uelewa wa masuala ya fedha pamoja na kuwaunganisha na taasisi zinazowainua vijana kimitaji.
Meneja Mwandamizi Kitengo cha Amana, Bima na Huduma za ziada wa Benki ya NMB, Bw. Stephen Adili (kulia) akizungumza na vijana katika kampeni zilizowakutanisha vijana na kujadili changamoto mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kuhamasisha vijana nchini kupata uelewa wa masuala ya fedha pamoja na kuwaunganisha na taasisi zinazowainua vijana kimitaji.
Mkurungenzi Mkuu wa UN
CDF Tanzania, Peter Malika (kushoto) akimkabidhi Meneja Mwandamizi Kitengo cha
Amana, Bima na Huduma za ziada wa Benki ya NMB, Bw. Stephen Adili (kulia) cheti
kilichotolewa na UN-CDF Tanzania, kwa NMB kwenye kampeni kuwahamasisha vijana
kupata uelewa wa masuala ya fedha wakiwa ndani ya banda la Benki ya NMB kujua
huduma anuai zinazotolewa na benki hiyo na kuwagusa vijana. NMB imeshiriki
kufanikisha kampeni hizo.
Baadhi ya wageni waalikwa
katika kongamano la kampeni zilizowakutanisha vijana kujadili changamoto
mbalimbali, wakipokea vipeperushi ndani ya banda la NMB kwenye kongamano hilo.
Baadhi ya wageni waalikwa
na vijana wakiwa katika kongamano la kampeni zilizowakutanisha vijana kujadili
changamoto mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kuwahamasisha kupata uelewa wa masuala
ya fedha.
Mwandamizi Kitengo cha
Amana, Bima na Huduma za ziada wa Benki ya NMB, Bw. Stephen Adili (kulia)
akifurahia cheti kilichotolewa na Mkurungenzi Mkuu wa UN CDF Tanzania, Peter
Malika (kushoto) kwenye kampeni kuwahamasisha vijana kupata uelewa wa masuala
ya fedha wakiwa ndani ya banda la Benki ya NMB kujua huduma anuai zinazotolewa
na benki hiyo na kuwagusa vijana.
Nikki Wa Pili (kushoto)
akizungumza na vijana walioshiriki kampeni zilizowakutanisha vijana kujadili
changamoto mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kuwahamasisha kupata uelewa wa
masuala ya fedha pamoja na kuwaunganisha na taasisi zinazowainua vijana
kimitaji.
Ofisa kutoka Ofisi ya
Waziri Mkuu, Idara ya Maendeleo ya Vijana, Eliakimu Mtawa (kushoto) akizungumza
na vijana walioshiriki kampeni zilizowakutanisha vijana kujadili changamoto
mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kuwahamasisha kupata uelewa wa masuala ya fedha
pamoja na kuwaunganisha na taasisi zinazowainua vijana kimitaji.
BENKI ya NMB imeshiriki
kampeni zilizoendeshwa na Shirika la Kimataifa la Mfuko wa Mtaji wa Maendeleo
UN- CDF zinazowakutanisha vijana pamoja na mashirika mbalimbali yanayofanya
kazi kuwahusisha maendeleo ya vijana. Kampeni hizo 'BankTheYouth'
zilizowakutanisha vijana na kujadili changamoto mbalimbali zinazowakabili
zimelenga kuhamasisha vijana nchini kupata uelewa wa masuala ya fedha pamoja na
kuwaunganisha na taasisi zinazowainua vijana kimitaji ili wafikie malengo
yao.
Akizungumza na vijana
walioshiriki kampeni hizo, Meneja Mwandamizi Kitengo cha Amana, Bima na Huduma
za ziada wa Benki ya NMB, Bw. Stephen Adili alisema vijana wanapaswa kuungana
katika vikundi na kuandaa maandiko ya biashara ambayo yataivutia benki kutoa
mikopo ili kuendesha biashara zao.
Alisema benki ya NMB
imekuwa mstari wa bele kuibua bidhaa mbalimbali za kibenki zinazolenga kuwainua
vijana hasa elimu ya uelewa masuala ya fedha na namna ya kujenga utamaduni wa
kujiwekea akiba. Aliwashauri vijana kutembelea matawi mbalimbali ya NMB na
kujenga urafiki kwa kufungua akaunti na kujiwekea akiba kabla ya kuanza
kunufaika na bidhaa mbalimbali zilizoanzishwa kuwasaidia vijana kimitaji.
"...Ili benki
ikuamini lazima ujenge mahusiano mazuri, ujenge urafiki na hii ni pamoja na
kuwa na akaunti na sisi. Hatuwezi kukuamini kama hata hauna akaunti na sisi,
anza kwa kujenga mahusiano mazuri kwanza nasi ndipo tukuamini...hatuwezi
kukukopesha kama haupo karibu na sisi," alisema Adili.
Kwa upande wake
Mkurungenzi Mkuu wa UN CDF Tanzania, Peter Malika aliwataka vijana kushiriki
vema katika kampeni hizo pamoja na kukubali kubadilika kulingana na mazingira
ya sasa na kutumia fursa zilizopo ili ziwaletee maendeleo. Aliwataka
kujadiliana na kuibua changamoto anuai ambazo zimekuwa vikwazo katika maendeleo
yao.
Alisema lazima wajiweke
katika vikundi na kufuata utaratibu mzuri utakaowekwa na taasisi zinazosaidia
vijana kuelekea katika maendeleo. Aidha aliongeza kuwa vikundi vya vijana
lazima vijulikane na kufuata utaratibu rasmi uliowekwa ili viweze kuaminika kwa
taasisi mbalimbali zikiwemo za kifedha. Aliwaomba wajiwekee utaratibu wa
kujiwekea akiba ili waweze kuaminika zaidi.
Naye Ofisa kutoka Ofisi
ya Waziri Mkuu, Idara ya Maendeleo ya Vijana, Eliakimu Mtawa aliwataka vijana kujenga
uaminifu wa kurejesha mikopo pale wanapopata fursa ya kukopeshwa kwani takwimu
zinaonesha fedha nyingi zinazotolewa na Serikali kuwakopesha vijana wapate
mitaji wamekuwa hawarejeshi jambo ambalo linatishia uhai wa mifuko hiyo
kuendelea kusaidia vijana wengine.
No comments:
Post a Comment