Mkuu wa Mkoa wa Tanga,
Martin Shighela (katikati), Balozi wa Norway wa kwanza kulia, Hanne-Marie
Karstand na Mganga Mkuu wa Mkoa, Asha Mahita (kushoto) wakifungua jengo la Afya
ya Akili hospitali ya Rufaa ya Bombo lililokarabatiwa na kituo cha Tanga
International Comperence Centre Tanga.
MKUU wa Mkoa wa Tanga, Martin Shighela, amesema
vita ya madawaya kulevya inaendelea hivyo kuviagiza vikosi vya ulinzi na
usalama kuhakikisha inawakamata vinara wa wasafirishaji na wauzaji.
Akizungumza katika hafla ya fupi ya makabidhiano ya
jengo la Afya ya Akili Hospitali ya Rufaa ya Bombo lililokarabatiwa na Kituo
cha Tanga International Comperence Centre (TICC), Shighela alisema vita ya
madawa itakuwa endelevu.
Alisema vijana wengi wamekuwa wakiathirika na
matumizi ya madawa ya kulevya na Taifa kukosa nguvu kazi ya kuleta maendeleo na
kuviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha Tanga hakuna njia ya upitishaji.
“Kuna wagonjwa wa akili kutokana na maumbile yao
lakini kuna wagonjwa wengine wa akili wa kujitakia ambao sababu zake ni
matumizi ya madawa ya kulevya” alisema Shighela na kuongeza “Ili kuwaokoa
vijana wetu na kupunguza nguvu kazi naviagiza vyombo vya ulinzi na usalama
kuongeza nguvu ya mapambano ya madawa ya kulevya” alisema.
Kwa upande wake Balozi wa Norway hapa nchini,
Hanne-Marie Karstand, amewataka watumishi wa hospitali ya Bombo kulitunza jengo
hilo kama ilivyo matumizi yake.
Alisema Serikali ya Norway itaisaidia Tanzania
katika Nyanja mbalimbali za kijamii ikiwemo Afya, elimu, Mazingira pamoja na
wagonjwa wa Afya ya Akili.
“Niuombe uongozi wa hospitali ya Bombo kulitunza
jengo hili kwa kutumika matumizi yake kama ilivyokusudiwa, Norway itaisaidia
Tanzania kila ambapo kunahitajika msaada” alisema.
Nae Mganga Mkuu wa Mkoa, Asha Mahita, alisema awali
wamekuwa wakikumbana na changamoto mbalimbali ikiwemo kukosa uwezo wa
kuwasafirisha wagonjwa kwenda vituo vinavyotoa huduma za Afya ya akili.
Aliwataka wafadhili wengine kuiga mfano wa Norway
kuisadia hospitali hiyo kutokana na changamoto ambazo imekuwa ikabiliana nazo.
Balozi wa Norway
hapa nchini, Hanne-Marie akiongea katika hafla ya fupi
ya makabidhiano ya jengo la Afya ya Akili Hospitali ya Rufaa ya Bombo
lililokarabatiwa na Kituo cha Tanga International Conference Centre (TICC),
Shighela alisema vita ya madawa itakuwa endelevu.
Sehemu ya wageni katika
hafla ya fupi ya makabidhiano ya jengo la Afya ya Akili Hospitali ya Rufaa ya
Bombo lililokarabatiwa na Kituo cha Tanga International Conference Centre
(TICC), Shighela alisema vita ya madawa itakuwa endelevu.
Sehemu ya wageni katika
hafla ya fupi ya makabidhiano ya jengo la Afya ya Akili Hospitali ya Rufaa ya
Bombo lililokarabatiwa na Kituo cha Tanga International Conference Centre
(TICC), Shighela alisema vita ya madawa itakuwa endelevu.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shighela akizungumza
katika hafla ya fupi ya makabidhiano ya jengo la Afya ya Akili Hospitali ya
Rufaa ya Bombo lililokarabatiwa na Kituo cha Tanga International Conference
Centre (TICC), Shighela alisema vita ya madawa itakuwa endelevu.
No comments:
Post a Comment