Akiongea jijini Dar es
Salaam mapema leo, Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania
PLC, Rosalynn Mworia amesema “Vodacom Tanzania PLC inatarajia kupokea maombi mengi ya kununua hisa
katika kipindi cha wiki hii.
Pia kutokana na ushauri
kutoka Serikali ya Tanzania na makundi mbalimbali muhimu ya kijamii
yanayohitaji kuwekeza wakiwemo Wabunge, makundi ya watumishi wa kada mbalimbali
wa serikali na maofisa wa vyama vya Ushirika kutoka sehemu mbalimbali za nchi,
tumewasilisha maombi na kupata idhini kutoka Mamlaka ya Soko la mitaji na
dhamana (CMSA) kuongeza muda wa zoezi la kuuza hisa kwa kipindi cha wiki tatu
hadi kufikia Alhamisi ya tarehe 11 Mei, 2017.
Mkurugenzi huyo alisema
kuongezeka kwa muda wa mwisho wa kununua hisa utawezesha wanaohitaji kununua
hisa kwa makundi binafsi na taasisi zilizoomba muda uongezwe kushiriki
kikamilifu katika mchakato huu. Tunatoa shukrani za dhati kwa watanzania ambao
wamejitokeza kuwekeza kupitia kununua hisa na tunawakaribisha ambao bado
hawajanunua hisa kuchangamkia fursa hii katika kipindi cha muda mfupi wa
nyongeza.
Mgawanyo na mchanganuo wa
umiliki wa hisa inapendekezwa utafanyika kuanzia Mei 19, 2017 na kuendelea
kabla ya kumaliza mchakato wa mwisho wa kujisajili katika Soko la Hisa la Dar
es Salaam katika tarehe iliyopangwa ya Juni 6, 2017.”
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria kwenye
mkutano huo.
No comments:
Post a Comment