Beki wa timu ya Simba SC Abdi Banda
ameaga rasmi jana baada ya timu yake kushinda Kombe la Shirikisho kwa kuipiga
bao 2 kwa moja Mbao FC katika mchezo uliofanyika mjini Dodoma.
Abdi
Banda anasema imefika wakati sasa anapaswa kutafuta maisha mengine nje ya klabu
hiyo au sehemu nyingine huku akisema atakumbuka mambo mengi mazuri katika klabu
hiyo
"Ahsante
Mungu nashukuru kwa hiki ulichotujaalia. Zawadi ya mashabiki wa Simba nawaachia
acha na mimi nitafute maisha sehemu nyingine. Nitamiss vitu vingi hasa
'support' yenu na moyo wenu wa uvumilivu ahsanteni sana na kwaherini" aliandika Abdi Banda.
No comments:
Post a Comment