Wakati Shirika la Afya Duniani WHO na Shirika la chakula
na Kilimo FAO likipendekeza kiwango cha unywaji maziwa kwa Binadamu ni lita 200 kwa mwaka,
imebainika kuwa nchi ya Tanzania unywaji wa maziwa kwa mwaka ni asilimia 47,
hii na sawa na chini ya robo ya kiwango kinachopendekezwa.
Kufuatia Ripoti hiyo
iliyotolewa na Mh Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo Na Uvuvi Mhe. William ole
Nashe (pichani) Serikali imejipanga kuboresha zao la maziwa kuanzia kwa Mfugaji
mpaka kwa mtumiaji, ili kuhakikisha zao hili linakuwa na Tija.
Akihutubia katika
Uzinduzi wa wiki ya Unywaji Maziwa Kitaifa
inayoadhimishwa Mkoani Kagera
katika Manispaa ya Bukoba, Mh. Naibu Waziri Ole Nasha amesema.
“Takwimu
Ya zao la maziwa nchini zinaonyesha kuwa,Nchi ya Tanzania huzalisha maziwa lita bilioni 2.1
kwa mwaka, ambapo 70% huzalishwa na Ng,ombe wa asili ambao uzalishaji wake ni
kati ya lita mpaka lita tano kwa siku, hata hivyo tunao ng,ombe wachache wa
maziwa wanakadiriwa kufikia Ng,ombe laki saba na elfu themanini na mbili ambao
wanakadiriwa huzalisha maziwa lita nane hadi ishirini kwa siku.”
Aidha Mh. Naibu waziri
William Ole Nasha, ameongeza kuwa “
maziwa yanayoingia viwandani kusindikwa kati ya maziwa yanayozalishwa ni 3% tu!, hapa nchini kuna
viwanda 75 vyenye uwezo wa kusindika lita
laki sita na Arobaini elfu kwa siku,
lakini kwa sasa viwanda vinavyosindika Maziwa ni 63 tu vyenye uwezo wa kusindika lita laki moja na elfu sitini na saba
na sabini za Maziwa kwa siku.
Hii ni sawa na wastani wa
unywaji wa maziwa, ni takribani lita 47 kwa
mwaka”
No comments:
Post a Comment