Tanga, SHEIKH wa Mkoa Baraza la Waislamu Tanzania (Bakwata) Tanga Juma Liuchu,
amewataka wafanyabiashara wa vyakula masokoni kuacha kupandisha bei za bidhaa
kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa Waislamu.
Akizungumza na
waandishi wa habari jana, Liuchu amesema Mwezi wa Ramadhani ni mwezi wa machumo
na baraka hivyo kuwataka kumuogopa Mungu ili kuepuka kupata dhambi.
Alisema
wafanyabiashara wengi hukitumilia kipindi cha mfungo wa Ramadhani kwa
kupandisha bei za vyakula hivyo kuwataka kuacha kufanya hivyo na badala yake
kuwapa unafuu wafungaji.
“Niwatake wafanyabiashara masokoni na madukani kuacha kupandisha bei za
vyakula, hebu tuogope kuingia katika dhambi na tuwape unafuu wafungaji” alisema Liuchu na kuongeza.
“Tamaa za pesa ndogo ndogo tena za muda mfupi zisitutoe katika imani na
tukawakomoa wafungaji na hili nitalifikisha katika tume ya kudhibiti bei za
bidhaa madukani” alisema.
Alisema kipindi
hiki cha mfungo wafungaji hutumia futari nyingi za nafaka hivyo kuwaasa
wafanyabiashara hao kutumia ubinadamu na kuacha kuwalangua.
Katika masoko
makubwa Ngamiani, Mgandini, Uzunguni na Makorora Mwandishi wa habari hizi
alitembelea na kujionea bei za bidhaa ikiwemo tambi ilikuwa zikuzwa 2,000,
kunde, 2,300, maharage 2,000, sukari 2,500 , nazi 800 na mchele ulikuw aukiuzwa
2,300 hadi 2,500.
No comments:
Post a Comment