Klabu ya nchini Uingereza ya Everton
inatarajia kutembelea Tanzania na kucheza mechi za kujiandaa na msimu mpya wa
2017/18.
Taarifa iliyoripotiwa na tovuti ya klabu hiyo imesema Everton
watatembelea Tanzania na itakuwa timu ya kwanza ya Ligi Kuu ya England kucheza
mechi katika nchi za Afrika Mashariki.
Ziara hiyo ambayo itakuwa sehemu ya sherehe zao za
udhamini mpya wa Kampuni ya SportPesa, itaifikisha Everton kwenye Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam wenye uwezo wa kubeba mashabiki 60,000 kucheza mechi
Alhamisi ya Julai 13.
Everton imemaliza ya saba katika msimamo wa Ligi Kuu ya
England ikijikusanyia jumla ya pointi 61 huku Chelsea ikimaliza ya kwanza kwa
kuwa na pointi 93 katika ligi hiyo inayoshirikisha timu 20.
No comments:
Post a Comment