BAHATI Nasibu ya Biko Ijue Nguvu ya Buku, sasa
imezidi kuchanja mbuga baada ya kuongeza donge nono la washindi wa droo zao
kubwa, ambapo sasa mshindi wa droo ya Jumatano hii anatarajiwa kunyakua jumla
ya Sh Milioni 20.
Mbali na kutoa kiasi hicho cha pesa, tayari
imempata mshindi wake wa droo ya tisa ya Jumapili ambaye ni Leopard Mpande wa
jijini Arusha, aliyenyakua Sh Milioni 10 huku pia Biko ikiwa imeshapata
washindi zaidi ya 35,000 wa papo kwa hapo.
Balozi wa Biko Tanzania Kajala Masanja kulia
akizungumza jambo wakati wa kuchezesha droo ya tisa ambapo mkazi wa Arusha,
Leopard Mpande aliibuka kidedea kwa kutangazwa mshindi hivyo atajinyakulia Sh
Milioni 10 kutoka Biko. Kushoto ni Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha
Tanzania, Jehud Ngolo.
Kajala Masanja akizungumza na Mwakilishi kutoka
Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Jehud Ngolo.
Mwakilishi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha
Tanzania, Jehud Ngolo kushoto akiandika dondoo za mshindi wa Sh Milioni 10 wa
Biko aliyetangazwa leo jijini Dar es Salaam, ambapo mkazi wa Arusha, Leopard
Mpande aliibuka kidedea katika droo hiyo.
Akizungumza leo katika
droo iliyompata Mpande, Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Biko, Grace Kaijage,
alisema kwamba wameamua kuongeza zawadi ya droo kubwa ya jumatano hii kutoka Sh
Milioni 10 hadi 20 ili kuwawesha washiriki nafasi ya kujikwamua kimaisha kwa
zawadi za BIKO, "Changamkieni fursa hii" alisema.
Alisema droo ya kumtafuta
mshindi wa Sh Milioni 20 itafanyika Jumatano, huku akiwataka watu wacheze mara
nyingi zaidi kwa kufanya miamala kwenye simu zao za MPESA, TIGOPESA na AIRTEL
Money kwa kuingia kwenye kipengele cha lipa bili au lipa kwa MPESA ambapo
watatakiwa waingize namba ya kampuni ambayo ni 505050 na kuweka pia namba ya
kumbukumbu ambayo ni 2456.
“Ukifanya
hivyo utaweka kiasi cha kununua tiketi kuanzia Sh 1000 au zaidi ambapo Sh 1000
itakuwa na nafasi mbili za ushindi kwenye droo kubwa ya Jumatano pamoja na
kushinda zawadi za papo kwa hapo kuanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000,
100,000, 500,000 na sh 1,000,000, huku donge kubwa likipanda kutoka Sh Milioni
10 hadi 20 Jumatano hii.
“Biko ni kutoa pesa kwa washindi wetu ili wafanikiwe katika maisha yao, hivyo wanachotakiwa kufanya ni kucheza mara nyingi, huku pia nikimpongeza mkazi wa Arusha, ndugu Mpande kufanikiwa kuibuka na Sh Milioni 10 katika droo iliyochezeshwa Jumapili,” Alisema.
Naye Mwakilishi wa Bodi
ya Michezo ya Kubahatisha, Jehud Ngolo, aliwapongeza Biko kwa kufikia hatua ya
kutoa Sh Milioni 20 kwa washindi wa droo kubwa ya Jumatano akisema ni hatua
nzuri, hivyo Watanzania wanapaswa kuchangamkia fursa hiyo ili waibuke na mamilioni
ya Biko.
“Sisi
tunafuatilia kwa karibu mchezo wa Biko na tunaridhishwa na utaratibu wao wa
upatikanaji wa washindi wa droo zao kubwa na ni mchezo wenye uaminifu mkubwa
hapa nchini ambapo wanatarajia droo ya Jumatano hii kutoa Sh Milioni 20, jambo
ambalo ni zuri kwa mustakabali wa kukuza uchumi kwa washiriki wote wa bahati
nasibu ya Biko,”
Alisema Ngolo na kumpongeza pia mshindi wa Arusha aliyeibuka na jumla ya Sh
Milioni 10,”
Alisema.
Kwa mujibu wa Biko, droo
ya Jumatano hii itatoa Sh Milioni 20, huku mshindi wao wa Arusha wa Sh Milioni
10 akitarajiwa kukabidhiwa fedha zake haraka iwezekanavyo kama walivyopewa
washindi wengine walioshinda katika droo nane za Jumatano na Jumapili
zilizopita.
No comments:
Post a Comment