Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na wadau wa Habari
kwenye Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani hapo katika Chuo cha
Habari Kilimani Mjini Zanzibar. Kushoto ya Balozi Seif ni Mkuu wa Mkoa
Mjini Magharibi Mh. Ayoub Mohamed Mahmoud, Katibu Mtendaji Baraza la Habari
Tanzania Bw. Kajubi Mukajanga, kulia ya Balozi Seif ni Mkuu wa Chuo cha Habari
Zanzibar Nd. Chande Omar na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni,
Utalii na Michezo anayesimamia Habari Nd. Hassan Mitawi.
Mkuu
wa Chuo cha Habari Zanzibar Nd. Chande Omar Omar akitoa ufafanuzi juu ya
Umuhimu wa Wanahabri kuzingatia suala la Amani katika uandishi wao wa kila
siku.
Viongozi
wa Meza Kuu kutoka kulia Katibu Mtendaji wa MCT Bw. Kajubi Mukajanga, Mkuu wa
Mkoa Mjini Maghribi Mh. Ayoub, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif,
Mkuu wa Chuo cha Habari Zanzibar Nd. Chande na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari
Nd. Hassan Mitawi wakifuatilia hafla ya maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari
hapo Kilimani.
Kikundi
cha Utamaduni cha Mkoa Mjini Magharibi kilitoa Burdani katika maadhimisho ya
Siku ya Uhuru wa Habari hapo katika Ukumbi wa Chuo cha Habari Kilimani Mjini
Zanzibar.
Katibu
Mtendaji Baraza la Habari Tanzania Bw. Kajubi Mukajanga akitoa salamu kwenye
hafla ya maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani Mjini Zanzibar.
Naibu Katibu Mkuu
Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo anayesimamia Habari Nd. Hassan
Abdulla Hassan Mitawi akifafanua jambo kwenye maadhmisho ya Siku ya Uhuru wa
Habari Dunani.
Mkuu
wa Mkoa Mjini Magharibi Mheshimiwa Ayoub Mohamed Mahmoud akijiandaa
kumkaribisha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif katika Maadhimisho
ya Siku ya Uhuru wa Habari yaliyofanyika katika Viunga vya Chuo cha Habari
Zanzibar kiliopo Kilimani Mjini Zanzibar.
Washiriki
mbali mbali waliohudhuria Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani
yaliyofanyika katika chuo cha Habari Zanzibar kilipo Mtaa wa Kilimani.
Balozi Seif Ali Iddi kati kati
waliokaa vitini akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi wa Taasisi
mbali mbali za Habari Nchini mara baada ya kufungua mdahalo wa maadhimisho ya
Siku ya Uhuru wa Habari Duniani. Kushoto ya Balozi Seif ni Mkuu wa Mkoa
Mjini Magharibi Mh. Ayoub Mohamed Mahmoud, Katibu Mtendaji Baraza la Habari
Tanzania Bw. Kajubi Mukajanga, kulia ya Balozi Seif ni Mkuu wa Chuo cha Habari
Zanzibar Nd. Chande Omar na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni,
Utalii na Michezo anayesimamia Habari Nd. Hassan Mitawi.
No comments:
Post a Comment