G
kwenye tarakimu hizi inawakilisha ‘Generation’, yaani kizazi fulani cha
teknolojia ya mawasiliano kwa kuangazia zaidi uwezo wa data kwenye simu.
Hakuna
kipimo chochote kinachotumiwa kimataifa kuhusu kasi ya data ya simu.Lakini
wengi wanakubaliana kuhusu baadhi ya sifa za teknolojia hizi.
Teknolojia
ya 1G, au kizazi cha kwanza cha data ya simu, ilianza kutumiwa 1991.
Teknolojia
ya 2G ilianza pia kutumika katika kipindi hicho, ikiwa kama ndugu wa 1G. Ambapo
kwa 1G, ungeweza tu kupiga simu.
Kisha 2G ikaja na uwezo wa kutuma
ujumbe mfupi au arafa
Teknolojia
ya 2G ambayo pia huitwa teknolojia ya SMS iliwezesha watu kutuma ujumbe
mfupi.Ungeweza pia kutuma ujumbe wenye picha, ambao uliitwa MMS (multimedia
messaging service). Na pia simu za wakati huo zilikuwa na teknolojia ya GSM,
GPRS, na EDGE.
Kupiga simu kwa video kuliwezekana 2001
3G
na kasi yake ya data ya 2mbit/s (megabaiti 0.25 kila sekunde) ilianza kutumika
wakati ambao simu za kwanza aina ya smartphone zilianza kuuzwa madukani.
Huduma
yake ya mtandao haikuwa ya kasi sana lakini iliwezesha huduma ya mtandao
kupatikana bila kutumia nyaya. Angalau ilikuwa hatua fulani. Na watu waliweza
kupiga simu za video.
Ili
kufahamu kasi yake au mwendo wake wa upole ulivyokuwa, iwapo ungetaka kupakua
filamu ya ucheshi yaDavid Brent: Life on the Road kutoka kwenye iTunes,
ingekuchukua saa tano kupakua faili hiyo ya 4.26GB.
2010 teknolojia ya 4G ikaanza kutumika
Teknolojia
hii ya kasi iliwezesha kuanza kupatikana kwa michezo mingi kwenye simu na ya
kiwango cha juu. Filamu ambayo ingekuchukua saa tano kuipakua kwa teknolojia ya
3G sasa inaweza ikakuchukua dakika 8 pekee kwa teknolojia ya 4G.
Lakini
4G haipatikani maeneo yote, hata katika mataifa yaliyoendelea. Afrika
Mashariki, utaipata katika baadhi ya maeneo ya miji mikubwa.
5G ndiyo mwendo kasi?
Tume
ya Mawasiliano ya Ulaya inakadiria kwamba kati ya mwaka 2020 na 2030, utaweza
kupakua filamu moja ya HD ya saa moja kwa sekunde sita pekee.
Simu
za wakati huo nazo zitakuwa na muonekano gani? Kama hii hapa chini labda?
No comments:
Post a Comment