Watafiti
wa Mikoa ya Kaskazini nchini wamegundua programu maalum ya simu itayomuwezesha
daktari ama muuguzi kutumia simu yake ya kisasa (smartphone) kusaidia
kuchunguza saratani ya kizazi, ugunduzi unaotajwa kuwa wa kipekee na wa kwanza
duniani.
Kwa
mujibu wa watafiti hao, daktari ama muuguzi katika kituo chochote anapaswa
kutumia simu yake ya kisasa baada ya kuunganisha (ku-install) programu hiyo
maalum, kupiga picha eneo la mfuko wa uzazi na kisha kutuma picha hiyo kwa
kutumia program hiyohiyo kwa mtaalam aliye kwenye kliniki husika.
Imeelezwa
kuwa baada ya kupokea picha kupitia program hiyo, wataalam wataichunguza na
kutoa majibu pamoja na maelekezo ya kitabibu kama ambavyo wangeweza kufanya
baada ya kupima mgonjwa husika.
Ili
kukwepa tatizo la uhafifu wa mtandao, muuguzi anaweza kupiga picha hiyo na
kuitunza kwenye simu na kisha kuituma pale mtandao utakapokuwa wa uhakika.
Program
hii inaonekana kuwa endapo itafanikiwa kwa kiwango kinachotarajiwa, itakuwa
msaada mkubwa katika kupambana na ugonjwa wa saratani ya kizazi nchini ambapo
zaidi ya wanawake 4000 wanadaiwa kupoteza maisha kila mwaka nchini kwa ugonjwa
huo, kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO).
No comments:
Post a Comment