Kiungo na Nahodha wa timu ya Simba SC,
Jonas Mkude amepata ajali baada ya gari waliokuwa wakisafiri nalo kupinduka
katika eneo la Dumila Mkoani Morogoro wakati wakirejea jijini Dar es salaam
kutokea Dodoma.
Jonas Mkude
Ajali hiyo iliyohusisha gari yenye namba za usajili T 834
BLZ, Toyota VX imetokea baada ya gurudumu la nyuma ya gari hiyo kupasuka na
kusababisha kifo cha mtu mmoja aliyetambulika kwa jina moja la Shose na majeruhi kadhaa
ambapo wamewahishwa kwenye hospitali ya Mkoa wa Morogoro kwa
ajili ya kupatiwa matibabu.
No comments:
Post a Comment