MAMLAKA
ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imesema wakati msimu wa mvua za masika
ukielekea ukingoni, wananchi wanatakiwa kufuatilia taarifa zinazoendelea
kutolewa ili kuchukua tahadhari dhidi ya mvua kubwa zinazoweza kutokea.
Msimu
wa mvua za masika ulianza Machi na zitamalizika Mei mwaka huu, katika maeneo ya
Ukanda wa Nyanda za Juu Kaskazini Mashariki katika mikoa ya Arusha, Kilimanjaro
na Manaya, Kaskazini, Pwani ya Kaskazini katika mikoa ya Morogoro, Pwani,
Dar es Salaam, Tanga na visiwa vya Unguja na Pemba.
Mkurugenzi
wa Utafiti na Matumizi ya Hali ya Hewa wa TMA, Dk. Ladislaus Chang’a,
alilieleza Nipashe jana kuwa mvua hizo zimeendelea kupungua wakati zikifikia
ukingoni.
“Mvua
zinaendelea kupungua, lakini matukio machache ya mvua kubwa yanaweza kuwatokea,
hivyo wananchi wanatakiwa kutufuatilia taarifa tunazotoa ili kuchukua tahadhari
ingawa zimepungua lakini hatuwezi kusema zimeisha hadi msimu umalizike,” alisema.
Alisema katika maeneo hayo na yale ya kuzunguka Ziwa Victoria wanapata mvua mara mbili kwa mwaka ambazo ni mvua za vuli na masika na kwamba kwa mwaka huu zilikuwa kubwa.
Alisema katika maeneo hayo na yale ya kuzunguka Ziwa Victoria wanapata mvua mara mbili kwa mwaka ambazo ni mvua za vuli na masika na kwamba kwa mwaka huu zilikuwa kubwa.
Alisisitiza
kuwa msimu wa mvua bado unaendelea, ingawa zinaelekea ukingoni
No comments:
Post a Comment