Matokeo ya sare ya kufungana 1-1 kati
ya Taifa Stars dhidi ya Lesotho, hayakuwa mabaya kwa mashabiki pekee, bali hata
kwa wachezaji na benchi lao la ufundi lakini nahodha wa Stars Mbwana Samatta
yeye alishindwa kuzuia hasira zake na kuonesha wazi kuwa alikasirishwa na
matokeo hayo.
Samatta amekiri mbele ya waandishi wa
habari kuwa, licha ya kutopenda kushindwa lakini hajafurahishwa na matokeo ya
kufungana 1-1 na Lesotho huku Stars ikiwa nyumbani mbele ya mashabiki wake
kibao.
“Mimi sipendagi kushindwa, hata draw
sijaifurahia kwa sababu tulikuwa tunacheza nyumbani na ukizingatia ni hatua ya
makundi tulikuwa tunahitaji ushindi kwa lazima kwa hiyo tumepata draw sio mbaya
lakini haikuwa katika akili yangu kwamba tupate draw dhidi ya Lesotho nyumbani
wakati tulikuwa tunahitaji ushindi ili kujitengenezea mazingira mazuri kwenye
kundi.”
“Nafikiri wachezaji wote walikuwa na
hasira sio mimi pekeyangu labda nilishindwa kujizuia kutoionesha lakini hakuna
mtu ambaye amefurahia matokeo haya.”
Lakini Sagoal amesema hata uwanja wa
Azam Complex umechangia Stars kushindwa kufanya vizuri kwa sababu ni mdogo na
ulikuwa unawanyima wachezaji nafasi hasa muda ambao Lesotho waliamua kutumia
mbinu ya kujilinda zaidi huku Stars wakitaka kushambulia.
“Ukiangalia uwanja wa taifa na Azam
Complex kuna tofauti, ukicheza kwenye uwanja wa taifa kuna kuwa na nafasi
zinaonekana lakini hapa (Azam Complex) kitu ambacho kimewasaidia Lesotho ni
uwanja kuwa mdogo kwa sababu waliweza kukaa nyuma na mipira yote ambayo ilikuwa
inapokelewa na wachezaji wetu mmchezaji wao mmoja au wawili walikuwepo. Kwa
hiyo mimi nafikiri uwanja umewasaidia.”
No comments:
Post a Comment