Spika Mstaafu Anna Makinda ameipongeza DCB
Commercial Bank kwa huduma bora za kibenki inayotoa hasa huduma za mikopo kwa
wajasirimali wadogo wadogo na kuwakwamua katika hali ya umasikini.
Makinda amewaasa DCB Commercial Bank kujikita
zaidi kutoa huduma hii kwa wajasiriamali wadogo wadogo vijijini ambao
ndiyo wengi nchini ili kuboresha hali za maisha yao kwa kuwapatia mikopo.
Hayo aliyasema wakati alipotembelea banda la
DCB Commercial bank katika maonesho ya nane nane kanda ya kati yanayoendelea
mkoani Dodoma. Makinda aliongezea kuwa ili kuwezesha wajasiriamali wengi DCB
Benki haina budi kupeleka huduma hii ya mikopo nafuu kwa wajasiriamali wadogo
wadogo vijijini ambako kuna uhitaji mkubwa wa huduma hii ya mikopo ya vikundi
Sambamba na utoaji wa mikopo hii ya vikundi kwa wajasiriamali wadogo wadogo.
Makinda ameasa DCB kuwaunganisha wajasiriamali
hawa na huduma ya bima ya afya kutoka NHIF na pia bima ya taifa ya Jamii ili
wateja hawa au familia zao wanapougua wapate msaada wa matibabu kwa unafuu
hivyo kuwafanya wawe na afya na kuweza kurejesha mikopo .
Alisisituza kuwa mteja akiugua ile pesa ya
marejesho ataitumia katika kugharamia matibabu hivyo kuitia hasara benki, kumbe
akijiunga na mifuko ya afya ya jamii atapata matibabu bure hivyo benki
haitaathirika. Alisema makinda.
Akimkaribisha kwenye banda na kuelezea huduma
zinazotolewa na DCB Commecral Bank, Meneja masoko wa DCB benki Boyd Mwaisame
alitaja huduma za DCB zinazopatikana katika banda la benki hiyo viwanja vya
maonesho nane nane Mzuguni Dodoma kuwa ni pamoja na kufungua akaunti za kuweka
akiba kwa watu binafsi, akaunti za wanafunzi, akaunti za muda maalumu, akaunti
za biashara na huduma za mikopo kwa wajasiriamali wadogo, wakati na
wakubwa.
Mteja akisha fungua akaunti ya akiba na
biashara anunganishwa bure na huduma ya DCB Pesa, huduma mpya ya kufanya
miamala ya benki kupitia simu ya mkononi, yaani kuweka na kutoa pesa na kulipia
bili mbalimbali. Huduma hii si lazima mteja awe na akunti DCB, bali mtu yeyote
mtaani anaweza kujiunga mradi tu awe na namba yoyote ya simu ya mkononi
iliyosajiliwa na mojawapo ya kitambulisha cha mpiga kura, utaifa, udereva na
paspoti.
Huduma hii inapatikana kwa kupiga *150*85#.
Pia Meneja masoko alimueleza Mh. Makinda kuwa huduma za DCB Commercial
Bank mbali na Dar es Salaam kwa sasa pia zinapatikana mkoani Dodoma kupitia
tawi lake lilifunguliwa hivi karibuni katika jengo la LAPF mtaa wa Makole
na mikoa mbali mbali kupitia huduma ya uwakala wa benki yaani DCB Jirani.
Naye afisa wa benki Cecilia Msikula
akimuelezea Mh. Makinda huduma ya akiba ya watoto akaunti za watoto –Young
saver account ambayo alivutiwa sana nayo hasa Meli ya mtoto, alisema kuwa DCB
inatoa huduma hii bila makato ya mwezi ambapo mteja akisha fungua akaunti ya
mtoto kwa shi. 5,000 tu anapewa Meli ya Mtoto/ kibubu bure kumjengea
mtoto utamaduni wa kujiwekea akiba akiwa bado mdogo kwa ajili ya matumizi yake
ya baadaye. Pesa ikisha jaa kwenye Meli ya mtoto yaani kibubu mzazi analeta
benki kwa ajili ya kuziweka kwenye akaunti ya mtoto baada ya kuzihesabu.
Katika msafara huo, Spika mstaafu Makinda
aliongozana na viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Mpwawa Mh. Jabir
Shekimweri.
Spika Mstaafu Anna
Makinda akikaribishwa na Mkuu wa Masoko wa benki ya kibiashara ya DCB Boyd
Mwaisame katika banda lao katika Maonesho ya Nane nane yanaoendelea Mkoa wa
Dodoma.
Spika
Mstaafu Anna Makinda akisoma moja ya kipeperushi cha benki ya DCB katika banda lao katika Maonesho ya Nane
nane yanaoendelea Mkoa wa Dodoma. Wa kwanza kulia ni Mkuu wa Masoko wa
benki ya kibiashara ya DCB Boyd Mwaisame.
Wananchi wakipatiwa
huduma katika banda la benki ya DCB katika Maonesho ya Nane Nane yanayoendelea
Mkoani Dodoma.
No comments:
Post a Comment