Chama
cha Wafanyabiashara Wanawake nchini TWCC kimekuwa mwenyeji wa wanawake
wajasiriamali kutoka nchi za Somalia, Chad na Sudan Kusini, ambao wapo
nchini kwa kozi ya mwezi mmoja, kwa ajili ya kujifunza shughuli mbali
mbali za ujasiriamali na uwezeshaji wanawake kiuchumi.
Mwenyekiti
wa TWCC Bi. Jacqueline Maleko amesema kwa kushirikiana na Shirika la
Kuhudumia Viwanda Vidogo Vidogo nchini SIDO, wamewapatia wanawake hao
mafunzo katika fani mbali mbali za ujasiriamali ikiwa ni pamoja na
kutembelea Chuo cha Uvuvi Mbegani ambako wamepatiwa mafunzo ya uokaji wa
samaki wabichi.
Kwa
upande wao, akina mama hao wameishukuru Benki ya Dunia iliyofadhili
mafunzo yao kutokana na umuhimu wake katika nchi zao ambazo kwa sasa
zina machafuko ya kisiasa ambayo yamekuwa yakiwazuia wanawake kupatya
ujuzi wa ujasiriamali.
No comments:
Post a Comment