SHEREHE YA MCHAPALO YA KUSHEREHEKEA MIAKA 54 YA MUUNGANO YAFANA WASHINGTON, DC - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Friday, April 27, 2018

SHEREHE YA MCHAPALO YA KUSHEREHEKEA MIAKA 54 YA MUUNGANO YAFANA WASHINGTON, DC

Mapokezi wakihakikisha kila mgeni anapokelewa vizuri na kwa ukarimu kwenye mchapalo wa kusherehekea sikukuu ya miaka 54 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliofanyika siku ya Alhamisi April 26, 2018, Washington, DC katika hotel ya Fairmont Washington na kuhudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo Waheshimiwa Mabalozi wanaowakilisha nchi zao nchi Marekani. Picha na Vijimambo Blog na Kwanza Production chini ya udhamini wa Kilimanjaro Studio.
Kulia ni Balozi wa Tanzania nchiniMarekani Mhe. Wilson Masilingi akifuatiwa na mkewe Marystela Masilingi wakiwa pamoja nae Mwambata wa jeshi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani na Canada, Brigedia Jenerali Adolph Mutta na mkewe wakijiandaa kupokea wageni waalikwa kwenye mchapalo wa kusherehekea sikukuu ya miaka 54  ya Muungano  wa Tanganyika na Zanzibar uliofanyika siku ya Alhamisi April 26, 2018, Washington, DC katika hotel ya Fairmont Washington na kuhudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo Waheshimiwa Mabalozi wanaowakilisha nchi zao nchi Marekani.
 Wageni wakiwasili huku wakisalimiana na Mhe. Balozi Wilson Masilingi, mkewe Marystela Masilingi,Mwambata wa jeshi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani na Canada, Brigedia Jenerali Adolph Muta na mkewe.
Mhe. Balozi Wilson Masilingi, Mkewe Marystela Masilingi, Mwambata wa jeshi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani na Canada, Brigedia Jenerali Adolph Mutta na mkewe wakipiga picha ya kumbukumbu na wageni waalikwa waliokuwa wakiingia ukumbini..
Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Wilson Masilingi na mkewe Marystela Masilingi wakiwa na mgeni wao. Bwn Eric Stromayer mwakilishi kutoka  Deperttment of State (Duputy AssistantSecretary Bereau of Africa Affairs ambaye ndiye aliyekua mgeni rasmi  wakiwa wamesimama kwa nyimbo za Taifa Tanzania na Marekani.
Mshereheshaji Julia Nyerere akisisitiza jamabo na kuelezea utaratibu wa kitu gani kinafuata
Balozi Mhe. Wilson Masilingi akisoma hotuba yake. Aliyelezea mambo mbalimbali ikiwemo kuitangaza Tanzania katika maswala ya utalii ikiwemo uhusiano mzuri kati ya Tanzania na Marekani. Katika hotuba hiyo Mhe. Balozi Wilson Masilingi aliongelea jinsi ya nchi ya Tanzania ilivyokua na amani na salama kwa watalii kwenda Tanzania kwenda kujionea vivutio mbalimbali na katika kuimarisha utalii, Serikali ya awamu ya tano chini ya Rasi Mhe. Dkt John Pombe Magufuli amenunua ndege sita za usafiri za ATCL zikiwemo tatu ambazo zimeshaanza kufanya kazi na zinginge tatu zitawasili ifikapo mwezi wa June mwaka huu ikiwemo ndege kubwaya Dreamline. Katika sherehe hiyo video ya vivutio mbalimbali zikiwemo mbuga zetu za hifadhi ya taifa zilikua zikionyeshwa.
 Bwn Eric Stromayer mwakilishi kutoka  Deperttment of State (Duputy AssistantSecretary Bereau of Africa Affairs ) akisoma hotuba yake na kuelezea uhusiano wa Marekani na Tanzania tangia zaiara ya baba wa taifa mwalimu Julius Nyerere alivyotembelea Marekani mwaka 1963 enzi hizo ikiongozwa na Rais John Kennedy.

Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Wilson Masilingi akiendelea kutoa hotuba yake.
Wageni waalikwa wakifuatilia hotuba ya Balozi Mhe. Wilson Masilingi.
Tosi ikifanyika.




Juu na chini ni Balozi Mhe. Wilson Masilingi, mkewe Marystela Masilingi, , Mwambata wa Ubalozi wa Tanzania na Canada, Brigedia Jenarali Adolph Mutta na mkewe wakipiga picha ya pamoja na wageni waalikwa walipokua wakiingia.






No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages