Mwenyekiti wa Uzalendo Kwanza Steve Mengele 'Steve Nyerere' akimsalimia Mzee Majuto ambaye amelazwa katika hospitali ya Tumaini jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Uzalendo Kwanza Steve Mengele 'Steve Nyerere' akiongea machache mara baada ya kumtembelea Mzee Majuto ambaye amelazwa katika hospitali ya Tumaini jijini Dar es Salaam.
Mzee Majuto akitoa shukrani zake mara baada ya kutembelewa na kuonyeshwa mwanga wa matibabu zaidi nchini India.
Msanii Aunty Ezekiel akimsalimia Mzee Majuto.
Kicheko kidogo...
Mtoto wa Mzee Majuto, Hamza akitoa shukrani kwa wasanii waliofika kumsalimia baba yake.
Mwenyekiti wa Uzalendo Kwanza Steve Mengele 'Steve Nyerere' akiteta jambo na Mzee Majuto.
Na Cathbert Kajuna
Msanii mkongwe wa filamu za vichekesho nchini, King Majuto anatarajia kupelekwa nchini India kwa matibabu kutokana na tatizo linalomkabili.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, mara baada ya kutoka kumsalimia Mzee Majuto ambaye amelazwa katika hospitali ya Tumaini, Mwenyekiti wa Uzalendo Kwanza Steve Mengele 'Steve Nyerere' amesema kuwa uamuzi huo umekuja baada ya kuona mzee Majuto amekuwa akihangaika mara kwa mara kutafuta matibabu.
"Tumeona mzee wetu anahangaika na matibabu ya mara kwa mara ambayo hayakamiliki sasa tumekuja na wazo la kumpeleka nchini India ili akatibiwe tatizo lake liishe na huu ndiyo wakati mwafaka wa watu tujitoe si mpaka mtu ashindwe kuongea tuanze michango," alisema nyerere.
"Jamani ifike wakati tujitoe kumsaidia mtu akiwa yupo hai na tusisubiri afariki ndiyo tuanze kuchanga, wakati ni sasa akiwa anaumwa tunamchangia anapatiwa matibabu na anaendelea na maisha," amesema Nyerere.
Tunamshukuru Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutuunga mkono kusaidia mwenzetu, pia Mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM Taiga (NEC) Salim Asas ambaye yeye amesema atatusaidia kwa hali na mali na ameanza kutupa tiketi 2 za ndege.
Tunataka mwenzetu akatibiwe maradhi yake yaishe aendelee na majukumu yake ya kujenga nchi na familia yake kwa ujumla.
Nyerere amewaomba wadau mbali mbali akiwemo Azam, DSTV na wengine wote wenye mapenzi mema kumsaidia mzee Majuto ili apone na aendelee na shughuli.
Kwa Upande wa Mzee Majuto amewashukuru watu wote ambao wamekuwa wakijitokeza kumsalimia na waendelee kumuombea ili apone.
"Sina cha kuwapa zaidi ni kuwaombea muendelee na moyo mlionao, mimi sina pingamizi kwenda kutibiwa nchini India, nipo tayari kamilisheni mipango yote mje kunichukua," amesema.
Ujumbe wa Steve Nyerere uliambatana na msanii mwenzake Aunty Ezekiel pia wakiwemo na waandishi wa habari wa mitandao ya jamii.
No comments:
Post a Comment