Zoezi la kuwasikiliza wakinamama Waliotelekezwa lafanikisha Watoto 2008 kupata uhakika wa Matunzo kutoka kwa Baba zao. - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Friday, April 27, 2018

Zoezi la kuwasikiliza wakinamama Waliotelekezwa lafanikisha Watoto 2008 kupata uhakika wa Matunzo kutoka kwa Baba zao.


Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mhe.Paul Makonda ametoa tathimini  ya Zoezi la kuwasikiliza wakina Mama  waliotelekezwa na kufikaofisini  kwake kwa lengo la kupata msaada wa kisheria lililokuwa likifanyika ofisi za mkoa huo na kumalizika leo ambapo lilifanyika takribani siku 15, mfululizo.

Akizungumza na waandishi wa Habari Makonda amesema zoezi hilo Idadi  ya kina Mama wamejitokeza ni  17,000 ambapo waliandikisha ni 7,000  ikiwa ni pamoja na wakina Baba 200 ambao walifika kutoa malalamiko yao, ambapo wataoto 2008 wamepata uhakika wa kupata fedha za matunzo kutoka kwa baba zao.

Amesema tatizo hilo ni kubwa katika jamii Jambo lililopelekea watoto kuwa omba omba, wanawake wanaotoa mimba na watupa vichanga pamoja na wanaotenda uhalifu wa kuiba pamoja na kuwa panya road, kutokana na kukosa matunzo kutoka kwa wazazi wao.

Amesema katika zoezi hilo wameweza kufanikiwa kusikiliza mashauri 7184, na kuwapatanisha  watoto 2008 waliopata uhakika wa matunzo kutoka kwa baba zao.

 "Tumesajili mafaili 7,184 ambayo tumeyasikiliza na kuyafanyia kazi ambapo familia 2008 wamepata uhakika wa kupata matunzo kutoka kwa baba zao, idadi hii ni kubwa sana kwani wamepata kuwafahamu baba zao na wengine kupata amani ya kuendelea kusoma wakipata huduma stahiki" Amesema Makonda.




Aidha amesema watoto ambao hawana uhakika wa wazazi wao watapatiwa bima za afya kwa ajili matibababu ambapo watoto 2,971 wamesajiliwa kupata huduma hiyo.

Ameainisha makundi matatu ya wakina Baba walioko katika mkoa huo na walipata taarifa ya wito,na kukaidi kufika tayari majina yao yamekabidhiwa kwa kamanda wa Polisi Lazaro Mambosasa ili kuchukuliwa hatua za kisheria,  na kundi la pili ni wale waioko nje ya mkoa huo,ambapo wametumiwa barua kupitia wakuu wa mikoa yao, pamoja na kundi la mwisho ambalo wakina Baba walioko nje ya nchi wametumiwa barua kupitia Waziri  wa ofisi ya Rais Tamisemi Suleiman Jaffo pamoja na mabalozi wao.

Ameongeza kuwa watoto wawili ambao ni wa wachina wameahidiwa kupata huduma za matunzo kutoka kampuni moja iliyopo hapa nchini ambayo inashulika na Ukandarasi ambayo ni ya wachina.

Aidha amewashukuru wanasheria, waandishi wa habari, na watu wote walioshiriki kikamilifu katika Zoezi hilo na kuwataka kuendelea na moyo huo ili kufanikisha maendeleo ya nchi ikiwa ni pamoja na kuanza kuboresha katika ngazi ya Familia.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages