Benki ya Exim Tanzania imetangaza kupata faida ya bilioni 9.6 kwa mwaka 2017, faida ambayo imewawezesha kuwa benki ya tano nchini.
Akizungumza na wanahabari kuhusu faida ambayo benki hiyo imeipata, Mkuu wa Kitengo cha Fedha wa Benki ya Exim, Seleman Ponda alisema faida ya mwaka jana imekuwa kidogo kulinganisha na mwaka 2016 ambapo ilipata faida ya bilioni 83.6 kwa sababu mbalimbali ikiwepo kuongeza mikopo ambayo haijafanya.
“Benki yetu imekuwa ya tano nchini ikiwa na rasirimali za trilioni 1.6. Kwa mtaji wa benki umeendelea kuimarika zaidi, hadi Desemba 2017 tulikuwa na Bilioni 231 kwahiyo tunao uwezo wa kukabiliana na majanga ambayo yanaweza kutokea,” alisema Ponda.
Aidha alisema kwa sasa benki imejipanga kuboresha huduma zaidi kwa njia ya mtandao kwani ni njia rahisi kuwafikia wateja wengi, kwa urahisi na kwa gharama ndogo zaidi tofauti na inavyotumika sasa.
Mkuu wa Kitengo cha Fedha wa Benki ya Exim, Seleman Ponda akizungumza kuhusu faida ambeyo benki hiyo imeipata kwa mwaka 2017.
“Huduma za digitali ndio lengo letu, kuna huduma nyingi tunafanya kwa mtandao, kwa digitali tunafikia wateja wengi zaidi na kupunguza gharama za uendeshaji. Kwa mwaka 2018 na kuendelea tumepanga kuboresha huduma kwa mtandao,” alisema
Pia alizungumza uwajibikaji kwa jamii (CSR), “Mwaka uliopita lengo ilikuwa kutoa vitanda na magodoro kwa hospitali mbalimbali nchini kama sehemu na kusaidia jamii. Sekta ya afya ni muhimu na kila mtu anahitaji kuwa na afya bora hivyo tuliona tusaidie huko.”
No comments:
Post a Comment