Mganga Mkuu wa Serikali-Wazara ya Afya, Prof. Mohammad Bakari Kambi, akiongea katika uzinduzi wa miradi mikubwa miwili (PAVIA na PROFORMA), inayolenga kuweka mifumo ya kuthibiti ubora na viwango vya madawa yanasambazwa na kutumiwa katika masoko ya Tanzania na nchi zingine za Afrika. (Picha na Mpiga Picha Wetu).
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA). Adam Fimbo, akiongea katika uzinduzi wa miradi mikubwa miwili (PAVIA na PROFORMA), inayolenga kuweka mifumo ya kuthibiti ubora na viwango vya madawa yanayosambazwa na kutumiwa katika masoko ya Tanzania na nchi zingine barani Afrika.
Mamlaka ya chakula na dawa nchini (TFDA) kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali Afrika jana wamebuni miradi miwili mikubwa yenye lengo ya boresha, kuhakiki na kufuatilia ubora na viwango vya madawa yanayosambazwa na kutumiwa na binadamu.
“Lengo kuu ni kumlinda mlaji na watumiaji wa dawa,” amesema Mganga Mkuu wa Serikali Kutoka Wizara ya Afya, Profesa Muhammad Bakari Kambi, wakati wa ufunguzi wa miradi ya PAVIA na PROFORMA, yenye lengo la kuweka mifumo ya kuthibiti ubora wa madawa barani Afrika. Miradi hii inafadhaliwa na Programu ya Maendeleo ya Majaribio ya Dawa Kwa Nchi za Ulaya na Afrika (EDCTP).
Akifafanua, Mganga Mkuu wa serikali amesema miradi hii itasaidia pia kufuatilia kwa urahisi madhara ya madawa yanayosambazwa na kutimiwa katika masoko.
‘’Miradi hasa itaweza kufanya ufuatiliaji matukio baada ya mgonjwa kutumia dawa husika na kuona ni kwa namna ipi imeweza kumsaidia au imemletea madhara baada ya kutumia ila hatua za haraka ziweze kuchukuliwa,’’ alisema Profesa Kambi.
Alisema kwamba miradi hii kwa pamoja itaweza kushughulikia usalama wa dawa kwa watumiaji na kufanya kwa kina udhibiti wa dawa bandia katika sehemu zote za nchini pamoja na maeneo ya mipakani.
Katika utekelezaji wa miradi hii kwa pamoja itatoa fursa kwa watumishi wa umma kujifunza jinsi miradi inavyoweza kufanya kazi na upatikanaji na utoaji wa taarifa muhimu tena kwa wakati katika kupambana na dawa bandia nchini.
Profesa Kambi aliongeza kwamba miradi inatarajiwa pia kuanza kubuni mitaala maalum itakayotumiwa na vyuo vikuu nchini katika juhudi za kuanza kuwandaa wanafunzi mapema jinsi ya kukabiliana na matokeo ya dawa kwa mgonjwa.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Dawa, kutoka Mamlaka ya chakula na dawa nchini, Adam Fimbo amesema usalama wa dawa nchini upo na mamlaka kupitia miradi hiyo miwili wataweza kuendelea kuboresha huduma za upatikanaji na udhibiti wa dawa hafifu na bandia katika soko la dawa nchini.
.
‘’Tumeungana na nchini kadhaa katika uanzishwaji na utekelezaji wa miradi hii katika harakati za kuweza kupambana matokeo baada ya mgonjwa kutumia dawa na kuweza kutengeneza mifumo inayoweza kuleta taarifa mapema na kuweza kuwasiliana kwa haraka na kubadilishana uzoefu,’’ aliongeza Fimbo.
“Sisi kama mamlaka ya chakula na dawa jukumu letu ni kusajili dawa, kuhakiki na kusiruhusu zitumike nchini lakini pia kuhakikisha tunafuatilia kwa karibu matokeo ya dawa kwa wagonjwa na tukigundua hazitowi matokeo chanya tunaziondoa mara moja,’’ alifafanua
Alifafanua kwamba miradi hiyo miwili inatasaidia kwa uhakika kutengeneza mifumo ya ufuatiliaji wa dawa kwenye soko na kuwajengea uwezo taasisi mbalimbali za afya nchini na kupelekea miradi hii kwenye mitaala ya vyuo vikuu.
Kwa upande wake, Afisa Mradi wa EDCTP, Bibi. Michelle Nderu alisema kwamba wameamua kufadhili miradi hiyo ili kuleta uzoefu kutoka kwenye nchini zilizoendelea ili kuboresha matumizi sahihi ya dawa kwa binadamu.
‘’Miradi hii itaweze kuongeza nguvu zaidi katika maeneo mengi katika nchini kadhaa chini ya jangwa la Sahara katika juhudi za kumlinda mgonjwa dhidi ya dawa bandia,’’ alisema.
Nderu aliongeza kwamba lengo la miradi hii ni kusaidia kuimarisha mifumo ya kitaifa ya afya kwa nchini za Afrika ili kuzalisha dawa mpya na zenye usalama na ubora wa uhakika na pia ufuatiliaji katika masoko.
Miradi ya PAVIA na Profoma inatekelezwa na kadhaa, ikiwa ni pamoja na Kenya, Italy, Uholanzi, Rwanda, Swedena na Ethiopia.
No comments:
Post a Comment