CCM WILAYA YA KUSINI UNGUJA YAKAGUA VITUO VYA AFYA JIMBO LA MAKUNDUCHI - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Wednesday, May 29, 2019

CCM WILAYA YA KUSINI UNGUJA YAKAGUA VITUO VYA AFYA JIMBO LA MAKUNDUCHI

MWENYEKITI wa CCM Wilaya ya Kusini Unguja Abdulaziz Hamad Ibrahim akiwa na Kamati ya Siasa wakikagua Sehemu ya Kuchomea Takataka (Kinu Moshi) za Kituo cha Afya Kibuteni katika ziara hiyo ya kukagua Utekelezaji wa Ilani.
MWENYEKITI wa CCM Wilaya ya Kusini Unguja Abdulaziz Hamad Ibrahim akizungumza na Uongozi wa Kituo cha Afya cha Kajengwa katika ziara ya Kamati ya Siasa ya Wilaya hiyo ya Kukagua Utekelezaji wa Ilani ya CCM katika Vituo vya Afya vilivyopo katika Jimbo la Makunduchi.
MWENYEKITI wa CCM Wilaya ya Kusini Unguja Abdulaziz Hamad Ibrahim akizungumza na Uongozi wa Kituo cha Afya cha Muyuni (hawapo Pichani) juu ya Ziara hiyo ya Kukagua Utekelezaji wa Ilani ya CCM katika Kituo hicho.


NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.

MWENYEKITI wa CCM Wilaya ya Kusini Unguja Abdulaziz Hamad Ibrahim, ameitaka Halmashauri ya Wilaya hiyo kutatua Changamoto zinazovikabili Vituo vya Afya katika Jimbo la Makunduchi ili kwenda sambamba na Matakwa ya Ugatuzi katika Sekta ya Afya Nchi.

Maelekezo hayo ameyatoa leo katika Ziara ya Kamati ya Siasa ya Wilaya hiyo ya kukagua Utekelezaji wa Ilani ya CCM ya Mwaka 2015/2020 katika Vituo vya Afya Vilivyomo ndani ya Jimbo la Makunduchi Unguja.

Alisema Serikali imefikia uamuzi wa kufanya Ugatuzi katika Sekta ya Afya kwa kuzipatia Mamlaka ya usimamizi Hslmashauri za Wilaya kwa lengo la kuimarisha Huduma za Afya ili Wananchi wapate huduma bora na kwa wakat mwafaka.

Mwenyekiti huyo aliipongeza Serikali kupitia Halmashauri ya Wilaya kwa wameimarisha upatikanaji wa Vifaa Tiba na huduma mbali mbali za msingi za Afya, lakini bado Vituo vingi vinakabiliwa na Changamoto ya Miundombinu Duni ya Majengo hali inayosababisha usumbufu kwa Wananchi na Watumishi wa Afya.

Abdulaziz alisema Uongozi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo wanatakiwa kufanya ziara za mara kwa mara katika Vituo vya Afya kwa lengo la kuratibu changamoto zinazovikabili Vituo hivyo ili viendelee kutoa Huduma Bora za Afya.

Katika maelezo yake Mwenyekiti huyo kwa niaba ya Kamati ya Siasa ya Wilaya hiyo, alimshukru Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein kwa kusimamia ipasavyo Mfumo wa Utoaji wa Huduma za Afya Bure kwa Wananchi.

“Tumetembelea Vituo vya Afya mbali mbali vilivyopo katika Jimbo la Makunduchi na kujionea namna vinavyotoa Huduma za Afya kwa Wananchi lakini pia tumebaini uwepo wa Changamoto ndogo ndogo na tumetoa maelekezo kwa wahusika zitatuliwe kabla ya Mwaka 2020.”alisema Mwenyekiti huyo wa CCM Abdulaziz.

Aidha alisema Chama Cha Mapinduzi Wilayani humo kitaendea kuisimamia Serikali itekeleze kwa ufanisi Ilani ya Uchaguzi hasa katika masusla ya utoaji wa Huduma za Afya ili kila Mwananchi apate fursa hiyo bila vikwazo.

Wakizungumza kwa Wakati tofauti Maafisa Utabibu wa Vituo vya Afya katika Jimbo hilo waliipongeza Serikali Kuu kwa kufanya Ugatuzi ambao umeongeza upatikanaji wa Huduma Bora za Afya kwa Wananchi wa Vijijini.

Maafisa hao walizitaja Changamoto zinazowakabili kuwa ni pamoja na Uchakavu wa Majengo ya Vituo, Ukosefu wa Uzio, Ukosefu wa Huduma za Usafiri kwa Watumishi wanaoishi mbali na Vituo hivyo, ukosefu wa Walinzi kwa baadhi ya Vituo.

Ziara hiyo imefanyika katika Vituo vya Afya vya Mtende,Kibuteni,Kizimkazi Mkunguni, Kizimkazi Dimbani pamoja na Muyuni.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages