GURU PLANET YATOA MAFUNZO YA MIFUKO MBADALA KWA WAJASILIAMALI - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Wednesday, May 29, 2019

GURU PLANET YATOA MAFUNZO YA MIFUKO MBADALA KWA WAJASILIAMALI

IKIWA zimebaki siku tatu za katazo la serikali la kutokomeza mifuko ya platiki (rambo) vikundi mbalimbali vya ujasiriamali vimeanza kutumia fursa hiyo kwa kutengeneza mifuko ya karatasi.

Kampuni ya Guru Planet iliyopo Tabata jana iliwakusanya wajasiriamali kwa kutumia mikono waliweza kujifunza na kutengeneza mifuko ya karatasi kwa lengo la kusambaza madukani na sehemu za biashara.

Akizungumza na waandishi wa Habari Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Nickson Martin alisema lengo kuwafanya wajasiriamali kujiari lakini pia kuendana na kasi ya kuacha kutumia mifuko hiyo ya rambo.

"Hapa wajasiriamali wengi baada kuona tangazo wamejitokeza na kuanza kujifunza kutengeneza mifuko hiyo ambapo tunamshukuru Mungu kwa hilo ila asilimia 90 ni akina mama na 10 akina baba kwa pamoja wataanza kupata masoko yaliyowazunguka mitaani mwao ili kuweza kuendana na kasi ya katazo,"

"Hata hivyo naamini soko ni kubwa mno hivyo kila mtu ajira hii imeanzia pale alipo na naamini watafanikiwa,"alisema Martini.Mwalimu wa mafunzo ya kutengeneza mifuko hiyo Bilhuda Mohamed alisema soko ni kubwa na huduma hiyo imeanzia kwa Dar es Salaam lakipi pia lengo kufika mikoani kote.

Wajasiriamali mbalimbali waliopata mafunzo hayo akiwemo Ester Sinduka (70) anasem alilisikia tangazo akiwa mkoani Mwanza na alipopata fursa kuja Dar es Salaam akaona ni vyema kujifunza ili akaweze kuwafundisha wajukuu zake jinsi ya kutengeneza mifuko hiyo.

Mafunzo hayo yameelewa kuwa na mwendelezo ambapo yatakuwa yanafanyika jumatatu,Alhamisi na jumamosi katika ofisi za Guru Tabata.
Mkurugenzi wa Tasisi ya Guru Planet, Nikson Martn akizungumza na Waandishi wa Habari wakati wa mafunzo ya utengenezaji wa mifuko mbadala kwa Wanawake wajasiliamali wa Mkoa wa Dar es Salaam
Mkurugenzi wa Tasisi ya Guru Planet, Nikson Martn akionyesha baadhi ya mifuko ambayo inatengenezwa na Wanawake Wajasiliamali
Mwalimu wa ujasiliamali kutoka Guru Planet,Bilhuda Mohamed, akionyesha baadhi ya vifaa vya kutengeneza mifuko mbadala.
Mwalimu wa ujasiliamali kutoka Guru Planet,Bilhuda Mohamed akiwa katika Mafunzo ya Vitendo na Wanafunzi na wanafunzi kutengeneza mifuko mbadala.
Wajasiliamali wakijifunza kwa vitendo namana ya kutengeneza mifuko mbadala

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages