MJASILIAMALI WA TWCC AELEZA NAMNA ALIVYOJIPANGA KUSHIRIKI MAONYESHO YA NANENANE - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Friday, July 17, 2020

MJASILIAMALI WA TWCC AELEZA NAMNA ALIVYOJIPANGA KUSHIRIKI MAONYESHO YA NANENANE

Mjasiliamali anaejishughulisha na kilimo Naomi Makandilo (wa kwanza kuhoto) akifafanua jambo huku akionyesha namna mbolea hiyo  inavyohifadhiwa.
Mjasiliamali anaejishughulisha na kilimo Naomi Makandilo (katikati) akitoa Elimu juu ya matumizi na faida za mbole ya Supergro wakati wa semina maalum ya iliyohusu mbolea hiyo.
 Zao la Nyanya (pichani)  lilivyositawi na kunawili likiwa shambani.
Zao la karoti (pichani) zikiwa shambani tayari kwa kuvunwa.

Dar es Salaam, Wajasiliamali wanaojishughulisha na kilimo cha Mazao mbalimbali yakiwemo ya chakula na biashara wameshauriwa kutafuta taarifa sahihi ya namna ya kupata pembejeo bora ili waweze kufaidikika kwa kupata mazao bora.

Mjasiliamali anaejishughulisha na killimo cha mazao mbalimbali yakiwemo Matunda na Mbogamboga Naomi Makandilo ametoa ushauri huo wakati wa mahojiano maalum  kuhusu mbolea ya kisasa ya kukuzia Mazao ya Super Gro inayotengenezwa nchini Marekani ambayo amekuwa akiitumia, amesema kuwa kuna kila sababu ya wakulima kuona umuhimu wa kutafuta taarifa juu ya mbolea hiyo ili waweze kupata faida katika kilimo chao.

Makandilo amesisitiza kuwa amejiandaa kikamilifu kushiriki Maonyesho ya Nanenane mwaka huu yatakayofanyika Kitaifa kwenye Mkoa wa Simiyu chini ya Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Tanzania (TWCC), na kwamba atatumia maonyesho hayo kuonyesha bidhaa hiyo sambamba na kutoa elimu kwa wakulima namna inavyofanya kazi.

“Super Gro ni Mbolea ya ukuzaji Mazao Shambani isiyo na viambata sumu, yenye kutunza unyevu na kufanya mazao kutokauka shambani, hii ndio bidhaa yangu nitakayokwenda nayo kwenye Nanenane Morogoro na Simiyu ndani ya chama cha TWCC, kama nilivyshiriki kwenye Sabasaba pia nitashiriki kikamilifu na maonyesho ya Nanenane mwaka huu.” Alieleza Naomi.

Aidha ameongeza kuwa uwepo wake ndani ya Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Tanzania (TWCC) kumemsaidia kuongeza wigo mpana zaidi wa kibiashara na kuwa na mtandao mzuri wa Wajasiliamali wenzake kutoka katika  Mikoa mbalimbali nchini.

“TWCC ni chama kizuri sana ndio mara yangu ya kwanza kuingia kwenye hiki chama na nimeona mwanga wa kibiashara ndio maana nimeamua kwenda nao Simiyu kwenye Maonyesho ya Nanenane” alisema.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages