TBS YAWAWEZESHA WAJASILIAMALI ZAIDI YA 600 KUPATA ALAMA YA UBORA BURE - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Sunday, July 5, 2020

TBS YAWAWEZESHA WAJASILIAMALI ZAIDI YA 600 KUPATA ALAMA YA UBORA BURE




Shirika la Viwango Nchini TBS limesema mpaka sasa limeweza kutoa alama za ubora kwa wajalisiliamali takribani 600 waliopitia mafunzo mbalimbali ya ujasiliamali chini ya Shirika la Viwanda vidogo Nchini SIDO.

Akizungumza kwenye mahojiano maalum Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano TBS Ryoida Andusamile amesema kuwa utaratibu huo wa kuwapatia Wajasiliamali alama ya ubora bila malipo yoyote umewawezesha wajasiliamali wengi kufaidika na huduma hiyo inayowapelekea kufanya kazi zao kwa kujiamini.

Aidha amesema kuwa kutokana na wajasiliamali wengi kuwa na mitaji midogo wengi wao walishindwa kufikia malengo yao na kutimiza ndoto zao na hivyo kujikuta wakishindwa kuyafikia masoko ya uhakika kutokana bidhaa zao kukosa alama hiyo muhimu kutoka TBS.

“wajasiliamali wakipitia kwenye mafunzo kule SIDO wakija kwetu wanapatiwa alama ya ubora bila malipo yoyote hii ni kutokana na Sera ya Serikali yetu ya awamu ya tano ya uchumi wa Viwanda tunataka kila Mjasiliamali awe na bidhaa bora ili aweze kuyafikia masoko makubwa, tunaamini atakapokuwa na alama ya ubora kutoka TBS anaweza kufanya biashara kwa kujiamini Zaidi” alisema Ryoida.

Amewata Wajasiliamali kote nchini watumie fursa hii kwa kufata utaratibu ulioweka ili waweze kufaidika na huduma hii inayolenga kumkwamua mjasiliamali na kumsaidia kuweza kupata alama ya ubora bila gharama yoyote.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages