WAJASILIAMALI WA KUTENGENEZA MAJIKO SANIFU WAELEZEA JINSI MRADI WA EnDEV ULIVYOINUA MAISHA YAO - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Monday, July 6, 2020

WAJASILIAMALI WA KUTENGENEZA MAJIKO SANIFU WAELEZEA JINSI MRADI WA EnDEV ULIVYOINUA MAISHA YAO


Msimamizi na Mshauri wa Mradi wa EnDEV unaotekelezwa chini ya Shirika lisilo la Kiserikali la Netherlands Development Organization (SNV) Rozalia Mushi wakwanza kulia akiwaonyesha wananchi waliotembelea banda lao kwenye maonyesho ya Sabasaba bidhaa ya Majiko sanifu yanayotengenezwa na wajasiliamali walipo chini ya Mradi huo.
Msimamizi na Mshauri wa Mradi wa EnDEV unaotekelezwa chini ya Shirika lisilo la Kiserikali la Netherlands Development Organization (SNV) Rosalia Mushi wakwanza kulia akielezea juu ya ufanisi na uhimara wa bidhaa ya Majiko sanifu yanayotengenezwa na wajasiliamali walipo chini ya Mradi huo.
Mjasiliamali na Mnufaika wa Mradi wa EnDEV unaotekelezwa chini ya Shirika lisilo la Kiserikali la Netherlands Development Organization (SNV) wakwanza kulia Bi Happyness Lenjinana mwenzake Shukuru Mesomapya wa pili kulia wakimuonyesha mteja jiko sanifu aliefika kununua bidhaa hiyo kwenye banda lao la maonyesho.
Bibi Fatuma Ramadhani Mjasiliamali na Mnufaika wa Mradi wa EnDEV kutoka Mvomero akielezea jambo wakati wa mahojiano maalum kuhusu namna alivyonufaika na Mradi huo wa jiko sanifu.
Bibi fausta Ntara kutoka Nyakato Mwanza wa kwanza kushoto mwenye fulana ya njano akiwa na Ofisa Mradi wa EnDEV wakizungumzia  ubora na usanifu wa jiko hilo liitwalo Matawi.

Zaidi ya wajasiliamali 100 wanaojishughilisha na utengenezaji wa Majiko sanifu ya kupikia wamepatiwa mafunzo na kupatiwa mitaji iliyowawezesha kujiendesha kibiashara katika wilaya 29 za Tanzania bara.  

Akizungumza kwenye maonyesho ya Sabasaba mshauri wa Mradi huo Rozalia Mushi amesema tayari mpaka sasa wamefanikiwa kuwafikia wajasiliamali 100 katika wilaya 29 za Tanzania bara kupitia Mradi wa EnDEV unaotekelezwa chini ya Shirika lisilo la Kiserikali la Netherlands Development Organization (SNV) lenye Makao yake Makuu nchini Uholanzi na kufanya shuguli zake nchini Tanzania.  

“Wajasiliamali wapo kwenye zoni nne ndani ya hizo Wilaya 29 ambapo tunawafikia kwaajili ya ushauri ya kibiashara na mafunzo ya jinsi ya kuzalisha bidhaa bora na kuwatafutia Masoko” alisema Rosalia.

Kwa upande wao wajasiliamali walioko kwenye maonyesho hayo ya sabasaba wamesema wanaushukuru Mradi huo kwani licha ya kuwasaidia kupata mafunzo ya kibiashara wameweza pia kunufaika kwa Elimu ya utunzaji wa Mazingira.

“kwakweli huu mradi umetutoa mbali sana kwanza kabisa wametufundisha namna ya kutengeneza majiko sanifu ya kisasa, wametuwezesha Mashine na vitendea kazi kiukweli ninashukuru sana” alieleza mjasiliamali Happiness Lenjima.

Wajasiliamali hao wapo kwenye maonyesho ya Sabasaba chini ya TWCC ikiwa ni siku ya pili toka yafunguliwe rasmi na waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Majaliwa kassim Majaliwa Julai 3, 2020.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages