Wednesday, November 3, 2021

Home
KITAIFA
LUHAGA MPINA APIGANIA BUNGENI BARABARA YA BARIADI - MWAUKOLI - MWANDU ITINJE- KABONDO - MWABUZO HADI IGUNGA
LUHAGA MPINA APIGANIA BUNGENI BARABARA YA BARIADI - MWAUKOLI - MWANDU ITINJE- KABONDO - MWABUZO HADI IGUNGA
Mbunge wa Kisesa, Mhe. Luhaga Mpina akiuliza swali la nyongeza bungeni Dodoma leo Novemba 3, 2021 kuhusiana na kupandishwa hadhi barabara ya Bariadi- Mwaukoli- Mwandu Itinje- Itinje- Kabondo- Mwabuzo hadi Igunga Tabora ambapo Serikali imekubali kufanya tathmini ya haraka ya barabara hiyo.
DODOMA | MBUNGE wa Jimbo la Kisesa, Mhe. Luhaga Joelson Mpina amehoji bungeni kuwa ni lini Serikali itaipandisha hadhi barabara ya kutoka Bariadi – Mwaukoli - Mwandu Itinje – Itinje – Kabondo -Mwabuzo hadi Igunga kuwa ya Mkoa baada ya TARURA kushindwa kuihudumia kutokana na ufinyu wa bajeti.
Akiuliza Swali la nyongeza bungeni Dodoma leo Novemba 3, 2021, Mhe. Mpina ametaka kujua mapendekezo yaliyowasilishwa serikalini kuhusiana na upandishaji wa barabara hiyo yaanza kutekelezwa lini ili kuwaondolea adha ya usafiri wananchi wanaotumia barabara hiyo muhimu kiuchumi inayounganisha Mkoa wa Simiyu na Mkoa wa Tabora.
“Asante sana Mh Spika kwa nafasi hii kwa kuwa barabara ambayo ameitaja Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo la Meatu, Mhe Leah Komanya ni barabara ambayo pia inaungana na barabara ya kutoka pale Mwabuzo ikaenda Kabondo, Itinje, Mwandu Itinje mpaka Mwaukoli na inaunganisha zote hizi inatoka Bariadi nyingine inatoka Meatu zinaenda zote Mkoa wa Tabora na Wilaya ya Igunga" Alisema.
"Sasa kwa sababu mapendekezo haya yote tuliyapeleka kwa pamoja kama ambavyo Naibu Waziri wa Ujenzi amejibu sasa anaweza kunihakikishia kwamba haya maombi yote yanafanyiwa kazi kwa pamoja na muda mfupi ujenzi utaanza wa mabarabara haya yatakuwa ya mkoa na baadae ujenzi kuanza mara moja ili kuondoa changamoto zilizopo kwa sasa za kutokana na Tarura kushindwa kumudu kukidhi mahitaji yake” amesema Mhe. Mpina
Akijibu swali hilo katika kipindi cha maswali na majibu bungeni Dodoma leo Novemba 3, 2021, Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhe. Mwita Waitara amemuagiza Meneja wa TANROADS Mkoa wa Simiyu kufanya tathmini haraka ya barabara hiyo na kuwasilisha wizarani majibu ili Serikali ianze mara moja ujenzi wa barabara hiyo.
“Mheshimiwa Spika naomba nijibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mpina kama ifuatavyo naomba nitumie Bunge lako tukufu Mheshimiwa Spika kumuagiza Meneja wa Mkoa wa Simiyu, Shinyanga na Mwanza na maeneo yote ambayo waheshimiwa wabunge wameshaleta mapendekezo katika maeneo haya wafanye kazi ya tathmini haraka iwezekanavyo wawasilishe majibu wizarani na sisi kama Serikali tuweze kuchukua hatua ili maeneo hayo yaweze kutengenezwa kwa haraka wananchi waweze kupata huduma ya barabara” amesema Mh. Naibu Waziri wa Ujenzi Waitara.
Tags
# KITAIFA
Share This
About Hassani Makero
Hassani Makero is a Wor'Out Media Country Manager located at Unguja-Zanzibar, Tanzania performing all technical issues concerning of Media Broadcasting activities, Satellites, and FM and Television equipments supplier.
Aside from that, Hassani Makero is also a Writer, Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 10 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs.
Aside from all above he own and operate his Blog known as Wor’Out Media since 2014.
Newer Article
TANZANIA NA UBELGIJI WATIA SAINI HATI YA MAKUBALIANO YA BIASHARA YA USAFIRI WA ANGA
Older Article
TUMIENI MBINU ZA KISASA KUIPENDEZESHA ZANZIBAR - MHE.OTHMAN
Zanzibar Afya Week yazinduliwa Dar es Salaam
Hassani MakeroApr 11, 2025SERIKALI YATOA MWEZI MMOJA KWA WANAFUNZI WA KIDATO CHA NNE 2024 KUBADILISHA MACHAGUO YA TAHASUSI ZA KIDATO CHA TANO
Hassani MakeroApr 02, 2025WADAU WAOMBWA KUJITOKEZA KUDHAMINI TAMASHA LA KUOMBEA UCHAGUZI MKUU MWAKA HUU
Hassani MakeroApr 02, 2025
Labels:
KITAIFA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment