Wednesday, November 10, 2021

Home
KITAIFA
SHERIA YA MISITU GN417 IMEENDELEA KUWA CHANGAMOTO KATIKA VIJIJI VINAVYOSHIRIKI DHANA YA USIMAMIZI SHIRIKISHI - WADAU
SHERIA YA MISITU GN417 IMEENDELEA KUWA CHANGAMOTO KATIKA VIJIJI VINAVYOSHIRIKI DHANA YA USIMAMIZI SHIRIKISHI - WADAU
Mkurugenzi Mtendaji wa MJUMITA Rahima Njaidi akizungumzia na wadau wa utunzaji Shirikishi wa misitu kutoka maeneo mbalimbali nchini.
Wadau wa utunzaji Shirikishi wa misitu wakisikiliza kwa makini hoja mbalimbali katika kikao Cha wadau wa usimamizi Shirikishi wa misitu.
Vumilia Kondo-Morogoro | IMEELEZWA kuwa sheria ya misitu GN417 imeendelea kuwa changamoto katika vijiji ambavyo vinashiriki dhana ya usimamizi shirikishi wa misitu (USMJ) nchini Tanzania.
Hayo yameelezwa na wadau wa misitu ambao ni wanachama wa Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu Tanzania (MJUMITA) katika kikao cha wadau wa usimamizi shirikishi wa misitu ya jamii.
Wamedai kwamba baadhi ya maeneo ambayo yalikuwa yakifanya USM kwa kutumia dhana ya uhifadhi misitu kupitia biashara endelevu ya mazao ya misitu wameanza kupoteza matumaini kutokana na kukosa wateja na upatikanaji wa fedha kupungua mwaka hadi mwaka.
Katibu wa Kamati ya Maliasili ya Kijiji cha Matuli kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro Sadiki Kondo amesema mapato ya Kijiji chao yameshuka ambapo kwa mwaka 2018/2019 Kijiji kilikukusanya Sh.milioni 80 huku 2020/2021 Kijiji Cha Matuli kimeweza kuvuna gunia 740 tu.
"Fedha tulizokuwa tunapata zilitusaidia kufanya Mambo mengi sana mfano Matuli tulichangia kujenga madarasa mawili ya shule ya msingi,kuwapatia wananchi CHF iliyoboreshwa Kijiji kizima,Kujenga matundu 20 ya vyoo shule ya msingi,kuchangua milioni 12 Sekondari na kuchimba visima sita vya maji..."
"Na kupata fedha ya uhifadhi kwa ajili ya msitu wetu wa Kijiji lakini katika mwaka 2021/2021 tumeshindwa kufanya chochote sababu mapato yameshuka hivyo GN 417 imetuletea changamoto hiyo hivyo wadau na Serikali waitazame upya," amesema Sadiki Kondo.
Kwa upande wake Ofisa Uwezesha kutoka Shirika la kuhifadhi misitu ya asili Tanzania Saimon Lugazo ameiomba Serikali kuingalia upya GN 417 kwa kuwa inaweza kuchochea uharibifu wa misitu katika maeneo ambayo wananchi walikuwa wakitunza misitu hiyo.
"Moja ya changamoto ni miongozo iliyotoka ya bei ya ushuru elekezi ya 12500 kwa gunia la mkaa kwa hiyo vijiji vinginambavyo havifikiki uzalishaji na mapato yameshuka sana, tunajua sheria ishapitishwa lakini inaweza ikatazamwa upya..."
"Kutokana na changamoto ambazo zimejitokeza,sababu wananchi wasipopata kitu Cha kuwashawishi wanaweza kubadilisha matumizi ya misitu na pengine kupelekea uharibifu kurejea tena," Lugazo.
Wakati huo huo Mkurugenzi Mtendaji wa MJUMITA Rahima Njaidi amewashauri wanachi kutoka maeneo mbalimbali ambayo kumekuwa na mkinzano wa sheria ndogo na sheria mama kukaa pamoja na kuzitathimi sheria hizo ili kuondoa mkanganyiko uliopo.
"Tumepokea.malalamiko kutoka maeneo mengi sana ya kukinzana kwa sheria ndogo za vijiji na sheria mama ambayo imekuwa ikirudisha nyuma Ari ya wananchi katika utunzaji wa misitu ya vijiji hivyo wake chini ili kuangalia namna gani wanamakiza mikinzano hiyo" amesema Njaidi.
Warsha hiyo imekusanya wadau kutoka maeneo mbalimbali ikiwemo Morogoro,Kilosa, Mvomero,Tunduru,Lindi, Liwale,Ruangwa na Iringa ambapo wadau wamepata nafasi ya kubadilishana ujuzi na uzoefu katika utunzaji wa misitu.
Tags
# KITAIFA
Share This
About Hassani Makero
Hassani Makero is a Wor'Out Media Country Manager located at Unguja-Zanzibar, Tanzania performing all technical issues concerning of Media Broadcasting activities, Satellites, and FM and Television equipments supplier.
Aside from that, Hassani Makero is also a Writer, Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 10 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs.
Aside from all above he own and operate his Blog known as Wor’Out Media since 2014.
Newer Article
RAIS SAMIA AELEKEA NCHINI MISRI KWA ZIARA YA SIKU 3
Older Article
Wananchi Wakimbilia Huduma Za NHIF Katika Maonesho Ya Wiki Ya Huduma Za Kifedha, Jijini Dar
Ni miaka minne ya neema kwa Mashirika ya Umma
Hassani MakeroMar 21, 2025INEC YATOA UFAFANUZI WANAOJIANDIKISHA ZAIDI YA MARA MOJA DAR
Hassani MakeroMar 20, 2025RAIS DKT. SAMIA ACHANGIA SH. MILIONI 50 KUMUENZI PADRI SHIRIMA
Hassani MakeroMar 20, 2025
Labels:
KITAIFA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment