WAZIRI BASHE AAGIZA WAZALISHAJI MICHE KUJISAJILI TOSCI - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Sunday, May 15, 2022

WAZIRI BASHE AAGIZA WAZALISHAJI MICHE KUJISAJILI TOSCI

Waziri wa Kilimo Hussein Bashe (katikati) akizungumza katika kongamano la uzinduzi wa mfumo wa usimamizi wa ubora wa miche na vipando lililofanyika jijini Dodoma mwishoni mwa wiki lililolenga kuhakikisha ubora wa miche inayozalishwa inaleta manufaa kwa wakulima kwa kufanya uzalishaji wenye tija sambamba na kudhibiti wazalishaji holela wa miche ya miti ya matunda nchini. Kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya kamati ya kudumu ya Bunge ya Kilimo,Mifugo na Maji, Dkt.Christine Ishengoma na kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Kuthibiti ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI), Bw.Patrick Ngwediagi.
Waziri wa Kilimo Hussein Bashe (katikati) akizungumza katika kongamano la uzinduzi wa mfumo wa usimamizi wa ubora wa miche na vipando lililofanyika jijini Dodoma mwishoni mwa wiki lililolenga kuhakikisha ubora wa miche inayozalishwa inaleta manufaa kwa wakulima kwa kufanya uzalishaji wenye tija sambamba na kudhibiti wazalishaji holela wa miche ya miti ya matunda nchini. Kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya kamati ya kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji, Dkt.Christine Ishengoma na kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Kuthibiti ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI), Bw.Patrick Ngwediagi.
Waziri wa Kilimo Hussein Bashe (katikati) akimkabidhi cheti uthibiti ubora mzalishaji wa miche ya parachichi kutoka Lusitu agro business Bw.Benno Mgaya (kulia) katika kongamano la uzinduzi wa mfumo wa usimamizi wa ubora wa miche na vipando lililofanyika jijini Dodoma mwishoni mwa wiki lililolenga kuhakikisha ubora wa miche inayozalishwa inaleta manufaa kwa wakulima kwa kufanya uzalishaji wenye tija sambamba na kudhibiti wazalishaji holela wa miche ya miti ya matunda nchini. kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Kuthibiti ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI), Bw.Patrick Ngwediagi.

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe ametoa miezi sita kwa wazalishaji wote wa miche ya matunda na vipando kuhakikisha wanajisajili kwa Taasisi ya Kuthibiti ubora wa mbegu Tanzania(TOSCI) kwa lengo la kuwatambua kuwasajili ili kufanya urahisi wa uthibiti katika uuzaji wa miche iliyo bora kwa wakulima nchini.

Miche ambayo imefanyiwa utafiti ni pamoja na miche ya miwa, parachichi, chikichiki, kakao, machungwa, korosho, ndizi , maembe, papai, kagawa, tofaa, chai na zabibu.

Waziri Bashe alizungumza hayo katika kongamano la uzinduzi wa mfumo wa usimamizi wa ubora wa miche na vipando lililofanyika jijini Dodoma mwishoni mwa wiki uliolenga kuhakikisha ubora wa miche inayozalishwa inaleta manufaa kwa wakulima kwa kufanya uzalishaji wenye tija sambamba na kudhibiti wazalishaji holela wa miche ya miti ya matunda nchini.

Natoa muda wa miezi sita kuhakikisha wazalishaji wote wa mishe na vipando wanasajili shughuli zao TOSCI, baada ya muda huo kupita wasiojisajili watafungiwa kufanya shughuli za uzalishaji miche nchini,” alisema Waziri

Alisema mfumo wa usimamizi wa ubora wa miche umeanzishwa kwa lengo la kuthibiti uzalishaji holela wa miche ambayo inapelekea wakulima wengi nchi kupata hasara kwa kununua mishe ambayo haina ubora au yenye sifa tofauti katika uzalishaji mazao.

TOSCI hakikisheni mnatembelea maeneo yote ya wazalishaji wa miche na vipando kwa lengo la kuwatambua, kuwapa elimu na kuwasajili ili waweze kuzalisha miche bora inayotakiwa na soko hii itafanya mavuno kuwa bora na kukubalika na soko,” aliagiza Waziri Bashe

Alisema TOSCI na Taasisi ya Utafiti wa mazao ya kilimo(TARI) zifanye tafiti ya ubora wa mbegu na miche inayotakiwa na soko ili kuhakikisha mkulima anapata mbegu bora itakayo leta mavuno kwa tija inayokubalika na soko.

Tukifanya hivyo tutakuwa tumejihakikisha kwamba sekta ya kilimo itaendelea kufanya mageuzi makubwa kwa kuongeza tija kwenye uzalishaji jambo litakalochochea zaidi uwekezaji katika viwanda vya kuchakata,kufungasha mazao kwa ajili ya kupeleka katika masoko ya ndani na nje ya nchi,” alisema

Alisema Serikali itaendelea kushirikiana na taasisi zake na wadau wa kilimo katika kuhakikisha sekta ya kilimo inaendelea kuchangia sehemu kubwa katika kutoa ajira kwa vijana katika mnyororo wa thamani wa kilimo na kupelekea taifa kupiga hatua kiuchumi na kimaendeleo.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa TOSCI, Bw.Patrick Ngwediagi amesema wataendelea kufanya uratibu kuhakikisha wazalishaji wote wanafata uratibu sheria na kanuni za nchi katika kufanya biashara ya miche na vipando.

Tumepokea maagizo ya Waziri na tutayafanyia kazi ili malengo ya kuanzishwa kwa mfumo wa usimamizi wa ubora wa miche yafanikiwe kwa kuhakikisha mkulima anapata miche yenye ubora ambayo itatoa matunda yanayokubalika sokoni,” alisema Bw.Ngwediagi

Meneja Mkazi wa Alliance for a Green Revolution in Africa (AGRA), Bw.Vianey Rweyendela amesema taasisi yake itaendelea kutoa ushirikiano kuhakikisha sekta ya mbegu inaboreshwa kwa lengo la kukuza kilimo nchini.

Kwa kushirikiana na SAGCOT, TAHA, TARI na wdau wengine katika sekta hii tutakwenda kuhakikisha tafiti zinaendelea kufanya juu ya mbegu bora zinazokubalika na soko,” alisema Bw.Rweyendela

Uzinduzi wa Mfumo wa Usimamizi wa Ubora wa miche na vipando umesimamiwa na TOSCI kwa uthamini wa Kituo cha Kuendeleza kilimo Nyabda za juu kusini mwa Tanzinia (SAGCOT), Alliance for a Green Revolution in Africa (AGRA) na Tanzania Agricultural Association (TAHA).

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages