Friday, March 8, 2024

MABORESHO RUVU CHINI MBIONI KUKAMILIKA
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Ndugu Kiula Kingu akizungumza na wanahabari wakati akitoa taarifa juu ya maboresho kuondoa tope kwenye Mtambo wa kuzalisha maji Ruvu Chini uliosababisha kupungua uzalishaji kwa asilimia 20.
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Ndugu Kiula Kingu (watatu kushoto), akionesha wanahabari namna wanavyotumia njiayakutoa tope kwenye Mtambo wa kuzalisha maji Ruvu Chini
Baadhi ya vijana wachapakazi wakisaidia kutoa tope kwenye Mtambo wa kuzalisha maji Ruvu Chini uliosababisha kupungua uzalishaji kwa asilimia 20.
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imesema kuwa kazi ya maboresho ya kuondoa tope kwenye Mtambo wa kuzalisha maji Ruvu Chini uliosababisha kupungua uzalishaji kwa asilimia 20 iko mbioni kukamilika.
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Ndugu Kiula Kingu ameeleza kupitia vyombo vya habari kuwa uchafu kwenye maji umesababisha tope kwenye machujio ya maji na hivyo kuathiri ubora na usafi wa maji yanayozalishwa kwenda kwa watumiaji.
"Tuliona ni vyema kutenga muda wa saa 36 kusafisha machujio ya maji ili kuwezesha kupatikana kwa maji yaliyo masafi na yenye ubora kwa watumiaji, amesema na kuongeza kuwa kazi ya kuondoa tope kwenye chujio kubwa ilianza tangu siku ya Jumanne na inafanyika usiku na mchana," amesema Ndugu Kingu.
"Mpaka sasa kazi imefikia hatua nzuri na leo jumatano zoezi la kuondoa tope itakamilika na kuruhusu baadhi ya pampu kuwashwa na huduma kurejea kwenye hali yake," ameeleza.
Ndugu Kingu ameeleza kuwa baada ya kukamilika kwa kazi hii huduma ya maji itaimarika na maji yaliyopungua kwa asilimia yanapatikana kwa usafi.
Ametoa wito kwa wananchi wote wanaoharibu miundombinu ya maji hasa kipindi hiki cha mvua kuacha mara moja kwa kuwa uharibifu unasababisha gharama kubwa kwa Mamlaka ya kusafisha mtambo kila mwezi tofauti na awali ambapo mtambo ulikuwa ukisafishwa kila baada ya miezi sita.
Tags
# KITAIFA
Share This
About Hassani Makero
Hassani Makero is a Wor'Out Media Country Manager located at Unguja-Zanzibar, Tanzania performing all technical issues concerning of Media Broadcasting activities, Satellites, and FM and Television equipments supplier.
Aside from that, Hassani Makero is also a Writer, Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 10 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs.
Aside from all above he own and operate his Blog known as Wor’Out Media since 2014.
Newer Article
MAGAZETINI LEO JUMAMOSI MACHI 9,2024
Older Article
HOW GEITA GOLD MINING EMPLOYS MORE WOMEN IN THE MINING SECTOR
SERIKALI YATOA MWEZI MMOJA KWA WANAFUNZI WA KIDATO CHA NNE 2024 KUBADILISHA MACHAGUO YA TAHASUSI ZA KIDATO CHA TANO
Hassani MakeroApr 02, 2025WADAU WAOMBWA KUJITOKEZA KUDHAMINI TAMASHA LA KUOMBEA UCHAGUZI MKUU MWAKA HUU
Hassani MakeroApr 02, 2025Rais Samia ahutubia Baraza la Eid El Fitr Jijini Dar es Salaam
Hassani MakeroMar 31, 2025
Labels:
KITAIFA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment