CRDB Insurance Na ACRE Africa Washirikiana Kuboresha Bima Ya Mifugo - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Wednesday, May 22, 2024

CRDB Insurance Na ACRE Africa Washirikiana Kuboresha Bima Ya Mifugo

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya CRDB Insurance, Wilson Mnzava akibadilishana hati ya makubaliano na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya ACRE Africa, Ewan Wheeler, katika hafla ya kusaini makubaliano ya kutoa huduma ya bima ya kilimo na mifugo, ambapo kwa kuanzia watanaanza na bima ya mifugo kwa kutumia teknolojia ya utambuzi pua za wanyama. Bima hii itapatikana nchi nzima kupitia matawi yote ya Benki ya CRDB. Hafla hiyo imefanyika leo Mei 22, 2024 jijini Dar es salaam.
 
Dar es Salaam, Tanzania, Mei 22, 2024 - Kampuni ya Bima ya CRDB 'CRDB Insurance Co' (CIC) na ACRE Africa wamesaini Mkataba wa Makubaliano (MOU) wa kutoa huduma ya bima ya kilimo na mifugo, ambapo kwa kuanzia wataanza na bima ya mifugo hapa nchini. 
 
Ushirikiano huu unaashiria hatua muhimu katika juhudi za pamoja za kuunga mkono jitihada za kuboresha sekta ya kilimo na kuboresha usalama wa chakula katika kanda.
Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika katika Makao Makuu ya CIC jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa CIC, Wilson Mnzava  alisema umuhimu wa ushirikiano huu ni Changamoto inavyosababishwa na mabadiliko ya hali ya hewa yanayoendelea kuathiri uzalishaji wa chakula na kusababisha hatari kubwa kwa maisha ya mamilioni ya wakulima na wafugaji, "CIC tunatambua uharaka wa changamoto hizi na tumejipanga kutoa suluhisho litakalowawezesha wakulima wetu na mifugo yao katika kukabiliana na hali hizi zisizo na uhakika," alisema Mnzava.
Mpango huu unalingana na mpango wa Serikali wa kukuza sekta ya fedha 2020-2030, ambao unalenga kuongeza ujumuishi wa bima nchini kufikia asilimia 50%. Makampuni ya bima yanahimizwa kubuni suluhisho la bima zinazokidhi mahitaji ya wateja na CIC iko mstari wa mbele katika mpango huu, ikitoa bidhaa za bima za kilimo zenye ubunifu, ikiwemo bima ya mifugo.

CIC, ni kampuni tanzu ya Benki ya CRDB, imejidhatiti kutekeleza mkakati wa kundi na kukuza kilimo nchini Tanzania. Mnzava alibainisha kwamba, "kwa kutumia mtandao wetu mkubwa wa matawi ya Benki ya CRDB na mawakala, tunaweza kufanya huduma hizi muhimu za bima zipatikane kwa wananchi wote. Ahadi yetu ni kuhakikisha kuwa wakulima kote nchini wanapata msaada wanaohitaji kulinda maisha yao, mazao yao, na kuchangia usalama wa chakula wa taifa."
Ushirikiano na ACRE Africa unadhihirisha jitihada za CIC katika wa kuunga mkono ajenda ya serikali na kutoa suluhisho kamili za bima zinazokidhi mahitaji ya sekta ya kilimo. "Ushirikiano huu unaashiria maono yetu katika kuleta mapinduzi katika sekta ya kilimo ambayo inatoa mchango mkubwa zaidi katika uchumi wa Tanzania," aliongeza Mnzava.

CRDB Insurance Company inatoa shukrani zake kwa wadau wote ambao wamechangia kufanikisha ushirikiano huu. Tunapoendelea mbele, tumejipanga kufanya kazi pamoja kulinda usalama wa chakula wa taifa na kuwaunga mkono wakulima na wafugaji wenye bidii ambao ni uti wa mgongo wa uchumi wetu.




No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages