Serikali kuendelea kushirikiana na Benk ya Absa kuendeleza nguvu kazi ya Taifa - Katambi - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Thursday, May 16, 2024

Serikali kuendelea kushirikiana na Benk ya Absa kuendeleza nguvu kazi ya Taifa - Katambi

Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu imesema itaendelea kushirikiana na uongozi wa Benki ya Absa nchini katika Programu ya Leaders in the Making "viongozi wa kesho". Program hiyo inalenga kuendeleza nguvukazi ya taifa hususani vijana kwa manufaa ya Benki hiyo na Taifa kwa ujumla.

Hayo yameelezwa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu wakati wa mahafali ya wahitimu waliofuzu katika Programu ya Leaders in the Making "viongozi wa kesho" leo tarehe 14 Mei 2024.

Mhe.Katambi amefafanua kuwa Programu hiyo inaunga mkono jitahada zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Serikali ya Awamu ya Sita katika Kukuza Ujuzi ambapo mafunzo imekuwa ikitoa mafunzo kwa wafanyakazi na watafuta kazi ili kukuza na kuendeleza ujuzi walionao.

Ameongeza kuwa Serikali inaitambua Programu hiyo kwa mchango wake mkubwa kwenye maendeleo ya nguvu kazi ya taifa na maendeleo ya taifa kwa ujumla hasa ukizingatia mazingira ya kazi yanabadilika haraka ambapo yanahitaji wahitimu kujiongezea ujuzi na uwezo wao zaidi.

Aidha; Mhe. Katambi ameyataka Mashirika mengine kuiga mfano wa Absa na kuzindua miradi kama hiyo kwa kujitegemea au kwa ushirikiano, kwani jukumu la kuwapa wahitimu ujuzi unaokidhi mahitaji ya kazi na ajira ni jukumu kubwa ambalo haliwezi kufanywa na Shirika moja peke yake au Serikali peke yake.

Awali akiongea katika Mahafali hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa, Bw. Obedi Laiser, amesema Programu hiyo ya ushiriki wa wahitimu inaendana na lengo kuu la benki ya Absa, ambalo ni Kuiwezesha Afrika na Tanzania yenye viongozi bora wa sasa na baadae.
Naibu Waziri Ofisi za Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu), Mhe. Patrobasi Katamb (wa pili kushoto), akikabidhi tuzo kwa mmoja wa wahitimu wa program ya Leaders in the Making ‘Viongozi wa Kesho’ iliyoandaliwa na Benki ya Absa Tanzania kwa kushirikiana na Kampuni ya Empower, Bi. Shanira Msale katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo. Wengine kutoka kushoto ni, Mkurugenzi Mwenza wa Empower, Bi. Miranda Naiman, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Bwana Obedi Laiser na Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Benki ya Absa, Bwana Patrick Foya.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages