DMI YASHIRIKI SIKU YA MABAHARIA DUNIANI - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Saturday, June 22, 2024

DMI YASHIRIKI SIKU YA MABAHARIA DUNIANI

CHUO Cha Bahari Dar es Salaam (DMI) kimeshiriki katika maonyesho ya siku ya mabaharia Duniani ambayo Kitaifa yanaadhimishwa katika viwanja vya Nia Njema vilivyopo katika Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani.

Maonesho hayo yaliyoandaliwa na Wizara ya Uchukuzi yamehusisha taasisi mbalimbali za serikali na wadau wa tasnia ya bahari yameanza Leo tarehe 22-25/06/2024 na yamefunguliwa na Mhe. Dkt. Khalid Salum Mohamed, Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Lengo la maadhimisho hayo ni kutambua mchango unaotolewa na mabaharia duniani na kitaifa hususani katika nyanja za kibiashara, uchumi na jamii kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages