Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa (kushoto) na Mkurugenzi wa Fedha wa Benki ya NBC, Waziri Barnabas (kulia) wakisaini makubaliano ya ushirikiano wa kiutendaji baina ya taasisi hizo mbili.
Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeingia makubaliano ya ushirikiano wa kiutendaji na Shirika la Reli Tanzania (TRC) yanatoa fursa kwa shirika kwa hilo kusafirisha washiriki wa mbio za NBC Dodoma Marathon kutoka jijini Dar es Salaam hadi Dodoma na kurudi kwa kutumia treni ya kisasa ya mwendokasi (SGR) ya shirika hilo.
Kupitia makubaliano hayo inatarajiwa kuwa washiriki zaidi ya 1,000 wa mbio hizo kutoka jijini Dar es Salaam watatumia usafiri huo wa haraka na wa kisasa zaidi ili kushiriki mbio hizo zitakazofanyika Julai 28 mwaka huu kwenye uwanja wa Jamhuri wa jijijni Dodoma. Lengo kuu la mbio hizo ni kukusanya fedha ili kusaidia mapambano dhidi ya saratani ya shingo ya kizazi na kutoa ufadhili wa elimu kwa wakunga ili kuboresha afya ya mama wa mtoto.
Hafla ya kusaini makubaliano hayo imefanyika mapema leo kwenye ofisi za TRC jijini Dar es Salaam ikihusisha viongozi waandamizi na maofisa wa pande zote mbili ambapo ilishuhudiwa Mkurugenzi Mkuu wa TRC, Bw Masanja Kadogosa na Mkurugenzi wa Fedha wa Benki ya NBC, Waziri Barnabas wakisaini makubaliano hayo kwa niaba ya taasisi zao.
Hafla hiyo ilitanguliwa na safari ya wadau hao kutoka jijini Dar es Salaam hadi Morogoro na kurudi hatua ambayo kutoa fursa kwa maofisa wa benki ya NBC na wadau wengine wakiwemo baadhi ya wakimbiaji kutoka vilabu mbalimbali vya wakimbiaji jijini Dar es Salaam kuweza kupata uzoefu wa usafiri huo kabla ya safari hiyo inayotarajiwa kufanyika siku moja kabla mbio.

Hassani Makero is a Softsol Mediatechnology Tanzania Ltd Country Manager located at Dar es Salaam-Tanzania performing all technical issues concerning of Media Broadcasting activities, Satellites, and FM and Television equipments supplier.
Aside from that, Hassani Makero is also a Writer, Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 10 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs.
Aside from all above he own and operate his Blog known as Wor’Out Media since 2014.
No comments:
Post a Comment