Biteko aikaribisha India kuwekeza miradi ya umeme jua nchini - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Monday, February 17, 2025

demo-image

Biteko aikaribisha India kuwekeza miradi ya umeme jua nchini

.tz/uploads/news/
  • Asema suala la Tanzania kuwa na nishati ya uhakika si la kusubiri.
  • Kampuni ya Kimataifa ya Umeme Jua (ISA) tayari imeonesha nia ya kuwekeza.
  • Kituo cha umahiri wa umeme jua kuzinduliwa Arusha Juni mwaka huu.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Kimataifa ya Umeme Jua (ISA), Bw. Ajay Mathur ya nchini India ambayo ameialika kuwekeza kwenye miradi ya umeme jua nchini.

Mazungumzo hayo kati ya Dkt. Biteko na Bw. Mathur yamefanyika jijini New Delhi nchini India ambapo pia Dkt. Biteko aliwasilisha mada katika mikutano mbalimbali ya Wiki ya Nishati India.

Tunawaalika mje kuwekeza Tanzania kwani tunahitaji kuwa na miradi mingi ya umeme kutoka vyanzo tofauti ili kuweza kutosheleza mahitaji ya watu wetu na kinachotupa msukumo zaidi kwa sasa ni mpango mahsusi wa misheni 300 tuliousaini mwezi Januari 2025 ambapo Tanzania tunapaswa kupeleka umeme kwa wananchi milioni 8.3 ifikapo mwaka 2030.” Amesema Biteko.
2
Dkt. Biteko ameishukuru kampuni ya ISA kwa kuona Tanzania kama sehemu sahihi ya uwekezaji na kueleza kuwa kazi yake ni kuhakikisha kuwa nchi inakuwa na miradi mingi ya nishati ambayo italeta utoshelevu wa umeme na kuchagiza maendeleo.

Kuhusu miradi ya umeme Jua nchini, Dkt. Biteko amesema Tanzania imeanza kutekeleza mradi wa umeme jua wa megawati 150 wilayani Kishapu mkoani Shinyanga kwa kuanza na megawati 50 ambapo megawati 100 zitaanza kutekelezwa baada ya kukamilika kwa awamu ya kwanza.

Ameongeza kuwa, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) pia limepata maeneo matatu kwa ajili ya miradi ya umeme jua ambayo ni Zuzu, Dodoma (MW 60), Mkwese, Manyoni - Singida (MW 199) na Same, Kilimanjaro (MW 50).
3..
Ili kuwezesha uwekezaji wa kampuni hiyo nchini, Dkt. Biteko amewataka Watendaji hao kuainisha maeneo ambayo wanahitaji kuwekeza ili Wataalam waanze kuyafanyia kazi.

Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya ISA, Ajay Mathur alimweleza Dkt.Biteko kuwa kampuni hiyo inataka kuwekeza kwenye miradi mikubwa ya umeme jua nchini huku msukumo wakiupata pia kutoka kwenye Mkutano wa Misheni 300 ambao ulieleza nia ya Afrika kufikisha umeme kwa watu milioni 300 Tanzania ikiwemo.

Amesema kampuni ya ISA inafanya kazi kwenye nchi 120 duniani na inashirikiana na Serikali mbambali katika utekelezaji wa miradi ya umeme juakwa njia mbalimbali ikiwemo kutoa mafunzo kwa wazawa kuhusu utengenezaji wa vifaa vya umeme jua, kusaidia serikali kutengeneza sera zinazowezesha uwekezaji katika nishati ya jua, kutoa maarifa kwa wahandisi wa nishati ya jua na watunga sera za nishati.
4
Katika hatua nyingine, Mathur amesema kuwa tayari kampuni ya ISA imeanza kufanya kazi Tanzania kwa kuwa na kituo cha Teknolojia ya Jua (STAR-C) ambacho kitakuwa na majukumu mbalimbali ikiwemo kuandaa mtaala na skimu za mafunzo sekta ya nishati ya jua na kuimarisha uwezo wa ndani wa kupima ubora wa vifaa vya jua kulingana na viwango vya kimataifa.

Vilevile kituo hicho kitasaidia ubunifu wa bidhaa na huduma zinazohimiza matumizi ya nishati ya jua, pamoja na kusaidia biashara katika mnyororo wa thamani wa sekta hiyo.

Ameongeza kuwa kituo hicho ambacho kimejengwa katika Chuo cha Ufundi Arusha kitazinduliwa mwezi Juni mwaka huu.

Kwa Afrika, ISA imeanzisha vituo vya STAR C nchini Ethiopia, Somalia, Ivory Coast na Ghana ambapo tangu kuanzishwa kwake vituo hivyo vimefundisha maelfu ya wataalamu katika sekta ya nishati ya jua.
5
Mazungumzo kati ya Dkt. Biteko na Bw.Mathur yalihudhuriwa na Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Anisa Mbega na Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Innocent Luoga.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages

Contact Form

Name

Email *

Message *