Wednesday, March 22, 2017

Home
KITAIFA
BENKI YA KCB TANZANIA YAZINDUA WARSHA YA BIASHARA CLUB KWA WATEJA WAKE AMBAO NI WAJASIRIAMALI WADOGO NA WAKATI
BENKI YA KCB TANZANIA YAZINDUA WARSHA YA BIASHARA CLUB KWA WATEJA WAKE AMBAO NI WAJASIRIAMALI WADOGO NA WAKATI
Benki
ya KCB Tanzania imeendelea kuwekeza kwa wajasiriamali wadogo na wakati kupitia
kitengo chake cha “Biashara Club”, kitengo kinachohudumia wajasiriamali wadogo
na wakati yaani (SME) kwa kuwapa huduma za kibenki na huduma endelevu za
kimaendeleo kwa wateja wake.
Zaidi
ya wanachama 100 wa Biashara Club wamekutana kujifunza jinsi ya kutunza fedha,
jinsi ya kufanya kwa vitendo uwekaji wa kumbu kumbu za hesabu , jinsi gani
taarifa ya fedha za biashara yako na taarifa za kifedha za mtu binafsi
zinavyokusanywa na kukaguliwa, na kwa njia gani taarifa hizi zinapatikana
kwenye taasisi za mikopo kupitia taasisi za kifedha.
Kwa
kuongezea, maelezo mafupi yalitolewa na Taasisi ya biashara, Viwanda na kilimo
Tanzania kuhusu utolewaji na uthibitishwaji wa vyeti halali kwa bidhaa zinazo
zalishwa hapa Tanzania, wao wamebobea katika kufanya tafiti mbalimbali nchi
nzima kwa kutumia mtandao wao na kuanzisha mfumo maalumu kwa wajasiriamali
wadogo na wakati,
kuzisaidia
taasisi za wajasiriamali wadogo na wakati, na kuwakutanisha wadau wa misitu kwa
pamoja na kufanya ushirika wa biashara kwa wadau na kuwaunganisha wanachama na
fursa zilizopo kwa washirika wa kibiashara wa kimataifa. Akiongea kwenye warsha
ya KCB Biashara Club iliyofanyika kwenye hoteli ya Hyatt Jijini Dar es
salaam,
Mkurugenzi
Mkuu wa KCB Bwana Godfrey Ndalahwa alisema kwamba, Benki ya KCB inatambua
umuhimu wa wajasiriamali wadogo na wakati katika kukuza uchumi wa nchi. “
Dhumuni letu sio kutoa suluhisho yakinifu kwa masuala ya kibenki tu bali pia ni
kuwapa ujuzi na nyenzo zinazohitajika katika kufanikisha biashara zao”
Wanachama wa KCB Biashara club watapatiwa ujuzi wa kutosha kupitia warsha
mbalimbali ambapo ushauri wa kibiashara utatolewa kutoka kwa wataalam waliothibitishwa.
Warsha
hizi zinatoa fursa kwa wajasiriamali wadogo na wakati kuwa kwenye mtandao na
kuwasiliana wao kwa wao na kushirikishina ujuzi bora wa kibiashara. Katika
kuongezea hili, pia wanachama watapata fursa ya kusaidiwa na mameneja uhusiano
wanaowasikiliza kwenye mahitaji yao ya kifedha. Wanachama wa KCB Biashara club
pia watanufaika na fursa zilizopo nje ya nchi ambapo matawi ya benki za KCB
yapo.
“
Ikiwa ni moja ya maidhinisho yanayotolewa na club hii, tumeweza kupata maelezo
kutoka kwa mtendaji wa KCB Biashara club Bwana Moses Odipo ambaye
ametushirikisha safari za kibiashara za mwaka 2017. Hii itawawezesha wanachama
wetu kushiriki kwenye safari za mkoa mpaka safari za kimataifa katika kuwezesha
biashara zao.Wanachama watahudhuria maonesho ya kibiashara ya Kimataifa ili
kujifunza jinsi wajasiriamali wengine wa kiwango chao wanavyo jiendesha kwa
dhumuni la kuboresha biashara zao .
Wakati
akitoa mchanganuo wa KCB Biashara Club, Bwana Masika Mukule, mkuu wa kitengo
cha wateja masuala ya kibenki, alisema kwamba, Biashara club imedhamiria
kuwawezesha wajasiriamali wadogo na wakati kwa kuwapa nyenzo na kuhakikisha
wana ujuzi sahihi wa kuendesha biashara zao na kutoa dondoo juu ya taarifa za
kifedha zinazohitajika na taasisi za kifedha pindi wanapo omba mkopo.
“Mwaka
huu warsha yetu ina maudhui mazuri sana yaliyoandaliwa kwa kufuata maoni
yaliyotolewa kwenye warsha yetu ya mwaka jana na tunaamini mwakani tutakuwa
tumewawezesha baadhi ya wajasiriamali wadogo na wakati kufikia kiwango cha
wateja wa kiwango cha juu.Bwana Mukule aliendelea kusema kwamba KCB wanazo
bidhaa mbalimbali kwa ajili ya soko la wajasiriamali wadogo na wakati ikiwa ni
pamoja na Masharti ya mkopo, overdaft facilities, Overdraft facilities, Bank
Guarantees, Invoice Discounting, Documentary letters of Credit, Asset Based
Finance na Bills Discounting.
Mbali
na hizi kitengo hiki kinatoa mikopo ya nyumba kwa wanao nunua, matengenezo au
kumalizia ujenzi, Advantage Banking na bidhaa za kibenki kwa wateja wetu
waliopo nje na ndani ya nchi .Wanachama wetu wana mengi ya kupokea kutoka kwetu,”
Alimalizia Bwana Mukule.
Mkuu wa Kitengo cha Kiislamu wa Benki ya KCB,
Rashid Rashid akitoa machache kwa wanachama wa Jukwa la Kibiashara 'Biashara
Club' iliyofanyika kwenye hoteli ya Hyatt Jijini Dar es salaam.
Mkuu wa kitengo kinachohudumia wajasiriamali wadogo
na wakati (SME), Edgar Masatu akiwakaribisha wageni waalikwa mbalimbali
waliofika kuhudhuria Warsha hiyo iliyoandaliwa na benki hiyo ya KCB mapema leo
jijini Dar.
Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya KBC, Godfrey Ndalahwa
akizungumza machache wakati wa warsha ya KCB Biashara Club iliyofanyika kwenye
hoteli ya Hyatt Jijini Dar es salaam leo.
Wanachama wa Jukwa la Kibiashara 'Biashara Club'
wakifuatilia kwa makini yaliyokuwa yakijiri ukumbi humo mapema leo.
Wanachama wa Jukwa la Kibiashara 'Biashara Club'
wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri ukumbini humo mapema leo asubuhi.
Tags
# KITAIFA
Share This
About Hassani Makero
Hassani Makero is a Wor'Out Media Country Manager located at Unguja-Zanzibar, Tanzania performing all technical issues concerning of Media Broadcasting activities, Satellites, and FM and Television equipments supplier.
Aside from that, Hassani Makero is also a Writer, Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 10 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs.
Aside from all above he own and operate his Blog known as Wor’Out Media since 2014.
Newer Article
KAIRUKI ATEMBELEA SEKRETARIETI YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA NA WALENGWA WA TASAF MKOANI MBEYA.
Older Article
BALOZI MERO AWASILISHA HATI ZA UTAMBULISHO
Rais Samia ahutubia Baraza la Eid El Fitr Jijini Dar es Salaam
Hassani MakeroMar 31, 2025MWENYEKITI WA CCM MKOA TANGA ASISITIZA AMANI SHEREHE ZA EID ELFITR
Hassani MakeroMar 30, 2025TCB BANK YAENDELEA KUIMARISHA UCHUMI WA MTU MMOJA MMOJA
Hassani MakeroMar 28, 2025
Labels:
KITAIFA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment