Saturday, March 25, 2017

TAASISI YA MANJANO FOUNDATION KUWAWEZESHA WANAWAKE WA MTWARA KIUCHUMI
Mradi wa Kuwawezesha wanawake Kiuchumi Kupitia Tasnia ya urembo
ujulikanao kama Manjano Dream-Makers ulioasisiwa na Taasisi ya Manjano
Foundation wataendesha mafunzo ya ujasiriamali kwa wanawake wa Mkoa wa Mtwara
kuanzia Jumatatu, tarehe 27 March 2017 kwenye ukumbi wa SIDO Mkoani Mtwara.
Mafunzo hayo yatatolewa kwa jumla ya wanawake watakaochaguliwa 30
kutoka mkoani Mtwara.
Baada ya mafunzo hayo wanaweke hao watakuwa chini ya uangalizi wa
Taasisi hiyo kwa lengo la kuhakikisha wanawake wa Mkoa wa Mtwara wanafikia malengo
yao waliojiwekea katika kujikita kwenye kujiajiri. Wanawake wakazi wa Mkoa wa
Mtwara waliotuma maombi kupitia tovuti ya Manjano Foundation na wanaopenda
kunufaika na mradi huo wanaombwa kujitokeza kwa ajili ya usaili siku ya
Jumamosi tarehe 25 Machi 2017 kuanzia saa tatu (9:00AM) asubuhi kwenye ukumbi
wa wa SIDO Mkoani Mtwara.
Mafunzo yana lengo la kumsaidia mjasiriamali mwanamke kujikwamua na
kujiongezea kipato. Awamu ya kwanza ni kumfundisha maswala ya biashara namna ya
kuibua na kubuni miradi mbalimbali namna ya kuandika mpangilio wa biashara
ikiwemo matumizi sahihi ya rasilimali muda, kutokufuja fedha na pia namna ya
kujitunzia akiba itokanayo na biashara yake.
Awamu ya pili itahusu kuwafundisha jinsi ya kupamba ma harusi na
matumizi sahihi ya vipodozi vya LuvTouch Manjano. Baada yanawake hawa kuhitimu
mafunzo haya Taasisi ya Manjano Foundation itawaunganisha na taasisi za fedha
zinazotoa mikopo bila riba waweze kupata mtaji wa kununua bidhaa za vipodozi
kwa ajili ya kuwawezesha kuanzisha biashara wakiwa chini ya uangalizi maalum
wa Taasisi hiyo kwa lengo la kuhakikisha kila mhitimu wa mafunzo haya
anapiga hatua na kuweza kujitegemea.
Wasiliana nasi kwa Simu namba +255
784 661 080 au +255 714 646 322
Tags
# KITAIFA
Share This
About Hassani Makero
Hassani Makero is a Wor'Out Media Country Manager located at Unguja-Zanzibar, Tanzania performing all technical issues concerning of Media Broadcasting activities, Satellites, and FM and Television equipments supplier.
Aside from that, Hassani Makero is also a Writer, Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 10 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs.
Aside from all above he own and operate his Blog known as Wor’Out Media since 2014.
Newer Article
KCB Bank conducts training to SMEs
Older Article
MARY NAGU UPBEAT ON KISHAPU WATER PROJECT
WAZIRI MKUU AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA MAJI MAKOREMO-MGONGORO
Hassani MakeroMar 12, 2025"Stori za Afya za Wanawake wa Tanzania zina thamani kwetu", Absa Bank
Hassani MakeroMar 12, 2025HALMASHAURI KUU YA CCM YAPENDEKEZA MAREKEBISHO YA KANUNI ZA UTEUZI WA WAGOMBEA UONGOZI
Hassani MakeroMar 11, 2025
Labels:
KITAIFA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment