TANAPA YAWAPA MAFUNZO YA UANDISHI WA HABARI NA UPIGAJI PICHA WAHIFADHI UJIRANI MWEMA NCHINI - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Wednesday, March 22, 2017

demo-image

TANAPA YAWAPA MAFUNZO YA UANDISHI WA HABARI NA UPIGAJI PICHA WAHIFADHI UJIRANI MWEMA NCHINI

_TM_2606







Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) katika kuhakikisha kuwa linaboresha mawasiliano yake baina ya wananchi wanaoishi maeneo jirani na hifadhi wameamua kuwapa mafunzo maalum ya wiki moja yanayolenga kuwajengea uwezo Wahifadhi Ujirani Mwema katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku hususan utoaji wa Elimu ya Uhifadhi kwa wananchi wanaoishi jirani na maeneo ya hifadhi nchini.Miongoni mwa mammbo ambayo wameweza kujifunza ni utoaji taarifa kwa njia ya habari. Ilikufanikisha hilo TANAPA imewapa mafunzo ya kitaalam maofisa wake hao katika mafunzo yanayoendelea mjini Dodoma. Pichani juu ni Mhariri wa Habari Mwandamizi wa Machapisho ya Mwisho wa wiki ya Gazeti la Habarileo, kutoka Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN), Oscar Mbuza akitoa mafunzo ya uandishi bora wa habari za kijamii kwa maofisa hao.

_TM_2597

_TM_2609

_TM_2611
Maofisa Uhifadhi Ujirani mwema kutoka hifadhi mbalimbali nchini wakifuatilia kwa umakini mafunzo hayo ya uandishi wa habari.
 


MAFUNZO+1



Maranyingi habari huendana na picha, ili somo hilo la Habari liwezuri na liende sawa maofisa hao pia walipewa mafunzo ya namna ya upigaji picha bora za Habari na namna ya kutumia Kamera. Mpigapicha Mwandamizi wa Magazeti ya Serikali (TSN), Mroki Mroki alitoa mafunzo hayo kikamilifu.



MAFUNZO+2



Muda wa majadiliano ulikuwepo baada ya kutoa mada, ambapo pia maswali yaliulizwa na kujibiwa.



_TM_2617

_TM_2612

_TM_2615

Washiriki wakifuatilia kwa umakini somo la upigaji picha.

_TM_2621
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA), Allan Kijazi nae alishiriki mafunzo hayo kama mwenyekiti wa mafunzo.
 

_TM_2619

_TM_2627

_TM_2622

                               Washiriki wakiendelea na mafunzo.
 

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages

Contact Form

Name

Email *

Message *