Msanii wa filamu nchini Yusuph Mlela amemtusi rapa Nay wa Mitego
kwa kile anachodai kuwa msanii huyo anapotosha jamii juu ya maandamano
waliofanya baadhi ya wasanii wa filamu nchini.
Yusuph Mlela ambaye kwenye post yake ameonekana kushindwa
kutumia lugha ya staha huku akionesha kutokwa na povu jingi kutokana na mapokeo
ya mashabiki wa filamu ambao walio wengi wamekuwa wakiwachana wasanii hao na
kuwataka kufanya kazi zenye ubora.
Rapa Nay wa Mitego alisikika akisema kuwa baadhi ya wasanii wa
filamu ambao waliandamana ni matahira kwani kitendo cha wao kutaka filamu za
nje zizuiliwe hakina tija na mantiki yoyote.
Kutokana na jambo hilo, ndipo hapo msanii huyo alipoamua
kushusha ujumbe kwa msanii Nay wa Mitego:
"Nay True Boy wewe jamaa si ulikuwa chocolaa wewe leo umeyapatia
kidogo unasahau kwamba nyuma yako kuna kundi la vijana wanatamani kuwa
waigizaji\wanamuziki wakubwa....acha kupotosha jamii yetu Kwa sababu zako
binafsi... sisi wasanii hatujakataza movie za nje. Tunataka wanaozisambaza
wafuate taratibu za kisheria ili uwiano wa biashara uwepo ndiyo lengo la
maandamano"alisema Mlela.
Mbali na hapo msanii huyo pia ameomba mpambano na Nay wazichape "Nay
wa Mitego acha kutafuta sifa... nakushangaa kuwa na ufikilivu mdogo kama wewe
siyo msanii...halafu huwezi kufananisha filamu na muziki.....
Wewe si mtoto wa Manzese unajifanya unajua kupiga ngumi nataka
Round 3 tu za boxing kwenye stage ili Tanzania ijue nani taahira nikutie
adabu..... This is serous coz we mtoto mdogo tu kwangu** kuongea sana tabia za
kike wewe si hip hop na unajiamini njoo uwanjani chagua popote pale"
Yusuph Mlela.
No comments:
Post a Comment