Mashabiki hao walikuwa wanatazama mechi kati ya Manchester United na
Anderlecht
Mashabiki wa soka
walikuwa wamekusanyika kwenye kituo cha kutazama mechi kupitia runinga katika
mji wa Calabar kusini mwa nchi hiyo mkasa ulipotokea.
Manchester United
walishinda 2-1 kwenye mechi hiyo ya hatua ya robofainali ligi ndogo ya klabu
Ulaya, Europa League.
Polisi nchini Nigeria
wamesema watu saba walifariki na wengine 10 wakajeruhiwa na wamelazwa hospitalini.
Mmoja yumo katika hali
mahututi.
Mwandishi mmoja nchini
humo ameambia BBC kwamba kisa hicho kilitokea baada ya waya wa umeme kuangukia
jumba.
Taarifa nyingine
zinasema kulikuwa na watu 80 kwenye jumba hilo wakati wa kutokea kwa mkasa huo.
Lakini baadhi
walifanikiwa kuondoka bila majeraha.
"Kufikia asubuhi, kulikuwa
na watu 7 waliokuwa wamefariki. Kuna 10 ambao wamelazwa hospitalini na mmoja
ambaye yumo chumba cha wagonjwa mahututi," walisema maafisa wa polisi.
“Kwa mujibu wa taarifa tulizopata kufikia
sasa, ni kwamba waya mkubwa wa umeme ambao ulikuwa karibu na jumba hilo
ulianguka."
No comments:
Post a Comment