Tuesday, May 2, 2017

KESI YA JAMII FORUM YAANZA KUSIKILIZWA
Melo na Mike wanadaiwa kuwa kati ya Aprili Mosi na Desemba 13, mwaka jana, huko Mikocheni wakiwa wakurugenzi wa Mtandao wa Jamii Media Co Ltd ambao unaendesha tovuti ya jamii forums wakijua jeshi la Polisi Tanzania linafanya uchunguzi kuhusiana na mawasiliano ya kimtandao yaliyochapishwa katika tovuti yake kwa njia ya kuuzuia uchunguzi huo walishindwa kutekeleza amri ya kutoa taarifa alizonazo.
Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu imetaarifiwa kuwa, amri ya kukamatwa kwa Mkurugenzi
mtendaji wa kampuni ya jamii Forums, ilitolewa na afisa Mkuu wa Upelelezi wa
Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SSP Ramadhan Kindai.
Kauli hiyo
imetolewa na yeye mwenyewe SSP Kindai wakati akitoa ushahidi wake mbele ya
hakimu Thomas Simba dhidi ya mkurugenzi mtendaji wa Jamii Forum, Maxence Melo
na Mwanahisa wa Kampuni hiyo, Mike William.
Shahidi huyo
wa kwanza wa upande wa mashtaka amedai, alitoa amri hiyo baada ya washtakiwa
kushindwa kutoa taarifa sahihi iliyochapishwa kwenye mtandao wa Jamii Forums..
Akiongozwa na
Wakili wa Serikali, Mohamed Salum, Kindai amedai kuwa waliomba taarifa kutoka
kwenye kampuni ya jamii Forums kutokana na kesi iliyofunguliwa na Afisa
Msimamizi wa mauzo ya rejareja wa Oil Com, Usama Mohammed.
Ameongeza
kuwa Usama alifika kwenye ofisi yao na kulalamika kuwa Februari 13, 2016 kuna
habari ilichapishwa kwenye mtandao wa Jamii Forums kwamba kampuni ya Oil Com
wanakwepa kodi bandari ya Dar es Salaam na kwamba wanaiibia serikali.
Amedai kuwa
katika kufuatilia kupata ukweli, ASP Fatuma Kigondo aliingia kwenye mtandao huo
kutafuta aliyechapisha taarifa hizo ambapo waligundua kuwa ni Fahara JF Expert
member ndiye aliyechapisha taarifa hiyo.
Kufuatia
hayo, Februari 23, mwaka Jana Kigondo aliandika barua kwenda kwa Mkurugenzi wa
Jamii forums ili awapatie taaarifa za mtu huyo ambapo walipokea barua toka
Jamii Forums ikidai kuwa wanahaki ya kulinda faragha za wateja wao.
Pia barua
hiyo ilikuwa ikitaka kujua tunaomba taarifa hizo kwa kifungu kipi cha sheria na
kwamba Majibu hayo hayakuwa chanya kwa kile walichokiomba.
Aliongeza
kuwa, waliandika tena barua Aprili Mosi, 2016 kuwakumbusha Jamii Forums kutoa
taarifa walizoziomba sababu kwa mujibu wa kifungu cha 10 (2) Cha Sheria ya
Mashauri ya Jinai (CPA) kinawapa mamlaka ya kuomba nyaraka kutoka katika ofisi
yoyote na lakini hawakujibu.
Amedai kuwa
kutokana na hayo waliona wanakosa haki ya kuendelea na upelelezi, na kuwa
wanawadhoofisha katika upelelezi wao ndipo wakaona wawakamate.
Kesi hiyo
itaendelea kusikilizwa kesho.
Tags
# KITAIFA
Share This
About Hassani Makero
Hassani Makero is a Wor'Out Media Country Manager located at Unguja-Zanzibar, Tanzania performing all technical issues concerning of Media Broadcasting activities, Satellites, and FM and Television equipments supplier.
Aside from that, Hassani Makero is also a Writer, Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 10 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs.
Aside from all above he own and operate his Blog known as Wor’Out Media since 2014.
WAZIRI MKUU AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA MAJI MAKOREMO-MGONGORO
Hassani MakeroMar 12, 2025"Stori za Afya za Wanawake wa Tanzania zina thamani kwetu", Absa Bank
Hassani MakeroMar 12, 2025HALMASHAURI KUU YA CCM YAPENDEKEZA MAREKEBISHO YA KANUNI ZA UTEUZI WA WAGOMBEA UONGOZI
Hassani MakeroMar 11, 2025
Labels:
KITAIFA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment