Friday, March 16, 2018

WANAVYUO NCHINI WAANDALIWE KATIKA KUJIAJIRI-MAJALIWA
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema ni umuhimu mfumo wa ufundishwaji wa wanafunzi wa vyuo vikuu nchini ukaboreshwa ili wanapomaliza waweze kujiajiri.
“Kumekuwa na tatizo kubwa la wasomi wetu kuwa na mtazamo kwamba wanapomaliza masomo yao lazima waajiriwe. Upo umuhimu wa kubadili mtazamo huo kwa kuwapa mbinu zitakazowawezesha kujiajiri.”
Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Ijumaa, Machi 16, 2018) alipokutana na kufanya mazungumzo na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Prof. William Anangisye, ofisini kwake mjini Dodoma.
Amesema wanafunzi hao wanapomaliza wanatarajiwa wawe na uwezo wa kubuni mbinu mbalimbali za kujiajiri na kuondokana na mtazao wa kusubiri ajira za kuajiriwa maofisini.
Waziri Mkuu amesema wasomi hao wanaweza kuchukua kauli mbiu ya Rais Dkt. John Magufuli ya uchumi wa viwanda kwa kuanzisha kilimo cha mazao mbalimbali yatakayotoa malighafi za viwandani.
Pia Waziri Mkuu amesema wasomi hao wanaweza kujikita katika shughuli za uchimbaji wa madini au usindikaji wa mazao mbalimbali, hivyo tayari watakuwa wamejiajiri kwa sababu ajira si za ofisini pekee.
Aidha, Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kumpongeza Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam aliyestaafu Profesa Rwekaza Mukandara kwa kazi nzuri aliyoifanya kipindi cha uongozi wake.
Kwa upande wake, Profesa Anangisye amesema mzigo aliopewa wa kuiongoza taasisi hiyo si mwepesi, hivyo ameahidi kufanya kazi kwa bidii na hatokwenda kinyume na matarajio ya Serikali ya Awamu ya Tano.
Kiongozi huyo amesema katika kuhakikisha wanaboresha masomo chuo hapo wameanzisha skuli ya kilimo na uvuvi, hivyo wanatarajia kuanzisha mashamba ya mfano kwa ajili ya mazao mbalimbali.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa(kulia) akizungumza na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Profesa William Anangisye(kushoto), ofisini kwa Waziri Mkuu mini Dodoma, Machi 16, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Profesa William Anangisye, ofisini kwa Waziri Mkuu mini Dodoma, Machi 16, 2018.
Tags
# KITAIFA
Share This
About Unknown
Hassani Makero is a Wor'Out Media Country Manager located at Unguja-Zanzibar, Tanzania performing all technical issues concerning of Media Broadcasting activities, Satellites, and FM and Television equipments supplier.
Aside from that, Hassani Makero is also a Writer, Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 10 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs.
Aside from all above he own and operate his Blog known as Wor’Out Media since 2014.
Newer Article
BALOZI WA KUWAIT NCHINI AKABIDHI MASHINE ZA WATOTO NJITI KWA TAASISI YA DORIS MOLLEL
Older Article
Mugabe appears on TV, condemns ‘Zimbabwean coup d’etat’
RAIS SAMIA AZINDUA JENGO LA HALMASHAURI YA MJI WA HANDENI
Hassani MakeroFeb 25, 2025SERIKALI ITAENDELEA KUJENGA MASOKO ZAIDI ILI KUTOA FURSA PANA YA KUFANYA BIASHARA KATIKA MAZINGIRA MAZURI.
Hassani MakeroFeb 25, 2025MAAFISA WA TUME YA UCHAGUZI WAFANYA ZIARA KATIKA VITUO VYA UANDIKISHAJI WAPIGA KURA ZANZIBAR
Hassani MakeroFeb 24, 2025
Labels:
KITAIFA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment