Kuna kipindi cha hapo awali kulikuwa na tetesi kuwa Lulu Diva alishapata mtoto huku awali lakini mtoto huyo amemuacha kwa mama yake na kwamba hataki watu wajue kama anamtoto, kitu ambacho Lulu Diva mwenyewe alikanusha na kusema kuwa amekuwa akikaa na watoto wa ndugu zake wengi kwahiyo hana mtoto wala hategemei kupata mtoto kwa sasa.
Akiongea na waandishi wa habari alipokuwa katika ufunguzi wa car wash ya Perfect Chrispin, Lulu Diva anasema kuwa kwa sasa amejikita kuwekeza zaidi katika kilimo kwa sababu kuna mashambe mengi ya mama yake ambayo ameachiwa na marehemu baba yake kwaio akiwa kama mtoto mkubwa kwenye familia yao ameona ni bora kuyafanyia kazi mashamba hayo.
No comments:
Post a Comment