Wednesday, May 9, 2018

RC MAKONDA AWAKEMEA WAKANDARASI AMBAO WANAJENGA BARABARA CHINI YA KIWANGO.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda amewaonya wakandarasi wenye tabia ya kutengeneza Barabara za chini ya kiwango na kuharibika ndani ya muda mfupi jambo linalosababisha hasara kwa serikali na usumbufu kwa watumiaji wa vyombo vya usafiri.
Makonda ametoa onyo hilo wakati wa hafla ya utiaji wa saini kwa Mikataba Nane ya mradi wa matengenezo ya Barabara, Mifereji ya Maji na Culvets inayotekelezwa na Wakala wa Barabara za Mjini na Vijijini TARURA yenye tahamani ya zaidi ya Billion 5.8 ambapo amewataka TARURA kuhakikisha wanasimamia ipasavyo ujenzi wa barabara hizo.
Aidha amezitaja Barabara zitakazojengwa kupitika mradi huo kuwa ni pamoja na Tegeta Nyuki, Msasani, Magomeni Makuti,Migombani, Kimara baruti, Kibanda cha Mkaa, Sheikh Bofu, Kwa Komba, Msigani, Sea clif na Mwananyamala Kisiwani.
Hata hivyo ametoa wiki mbili kwa TARURA kuhakikisha wakandarasi waliojenga barabara chini ya kiwango zinajengwa upya kwa gharama ya mkandarasi ikiwemo barabara ya Mabatini ambapo barabara hizo zitakuwa na mifereji ya maji, sehemu za watembea kwa miguu na Taa za Barabarani.
Pamoja na hayo Makonda amesema katika uongozi wake hawezi kufumbia macho matumizi mabovu ya fedha za walipa kodi hivyo atahakikisha anasimama kidete kuhakikisha Dar es salaam inakuwa na barabara zenye ubora.
Sanajari na hayo Makonda ametaka uwepo wa ushirikiano wa kikazi baina ya TARURA, TANROAD, TANESCO, DAWASCO na TTCL ilikupunguza ucheleweshaji wa miradi na ujenzi usiofuata taratibu unaopelekea uharibifu wa miundombinu.
Tags
# KITAIFA
Share This
About kilole mzee
Hassani Makero is a Wor'Out Media Country Manager located at Unguja-Zanzibar, Tanzania performing all technical issues concerning of Media Broadcasting activities, Satellites, and FM and Television equipments supplier.
Aside from that, Hassani Makero is also a Writer, Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 10 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs.
Aside from all above he own and operate his Blog known as Wor’Out Media since 2014.
KILUPI: ATAKA KURA ZA MAONI ZISIWAGAWE WANACCM
Hassani MakeroApr 14, 2025Dkt.Dimwa - Akemea Rushwa Mchakato wa Kura za Maoni
Hassani MakeroApr 14, 2025WAZIRI ULEGA AWAOMBA TET KUENDELEZA TUZO YA TAIFA YA MWALIMU NYERERE YA UANDISHI BUNIFU
Hassani MakeroApr 14, 2025
Labels:
KITAIFA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment