RAIS wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Mhe.Dk Ali Mohamed Shein amewataka wahitimu wa Chuo cha Abdul Rahman Al Sumait kutumia ujuzi walioupata chuoni hapo kwa kujiajiri wenyewe bila ya kusubiri ajira kutoka Serikalini.
Akisoma hotuba kwa niaba yake huko Chukwani, katika mahafali ya 18 ya chuo hicho, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe.Riziki Pembe Juma amesema tatizo la upungufu wa ajira si la Serikali ya Mapinduzi Zanzibar pekee bali ni kilio cha dunia nzima.
Aidha Dk. Shein ameupongeza uongozi wa chuo cha Alsumait kwa kuzalisha walimu bora na wenye vigezo ambao wanasaidia kuwasomesha watoto katika skuli za serekali na binafsi.
Pia katika risala hiyo Dk. Shein ameutaka uongozi wa Abdul Rahman Al Sumait kuongeza nafasi za udhamini wa masomo kwa vijana wa Zanzibar ambazo zitaisaidia kua na wasomi wengi wa Elimu ya juu pia kutanua mashirikiano baina yao.
Nae Mwenyekiti wa Alsumait Dk. Abrahman Al Muhailan amesema chuo kimekuwa na malengo ya kuhakikisha kinatoa elimu yenye ubora Kama ilivosisitizwa katika qur_an tukufu kuwa "kutoa kilichobora kwa wengine ni sawa na sadaka inayoendelea ambayo malipo yake ni duniani na akhera.
Kwa upande wake Makamo Mkuu wa Chuo cha Al Sumait bwana Amran Rasli amewasisitiza wahitimu hao kurejesha mikopo waliopatiwa ili waweze kupatiwa na wengne waweze kusoma.
No comments:
Post a Comment