RC MAKONDA ARIDHISHWA NA KASI YA UJENZI WA MACHINJIO MAPYA YA VINGUNGUTI, ATOA MAAGIZO MATATU MAZITO MANISPAA YA ILALA - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Sunday, September 29, 2019

RC MAKONDA ARIDHISHWA NA KASI YA UJENZI WA MACHINJIO MAPYA YA VINGUNGUTI, ATOA MAAGIZO MATATU MAZITO MANISPAA YA ILALA


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda ametembelea na kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Machinjio ya kisasa Vingunguti ikiwa ni mkakati wake wa kufuatilia bila kusubiri kuletewa taarifa ofisini ambapo amewapongeza Shirika la Nyumba la Taifa NHC kwa kufanya Kazi Usiku na Mchana kwa lengo la kuhakikisha ujenzi huo unakamilika ndani ya Miezi mitatu kama ilivyo Matarajio ya Rais Dkt. John Magufuli.

Katika ziara hiyo RC Makonda amemuelekeza Mstahiki Meya wa Ilala Bw. Omary Kumbilamoto kuja na Mpango wa kuhakikisha miundombinu ya Reli inaunganishwa kwenye machinjio hayo ili Treni iweze kutumika kupokea wanyama na kusafirisha nyama ndani na Nje ya Nchi.

Aidha RC Makonda amemuelekeza Meya huyo kuhakikisha ujenzi wa Barabara ya Vingunguti unaanza Mara moja huku akiitaka Manispaa ya Ilala kufikiria uwezekano wa kulipa fidia kwa wakazi wanaozunguka machinjio hiyo ili kwa miaka ijayo machinjio iweze kupanuliwa na kuwa kubwa zaidi.

Pamoja na hayo RC Makonda amesema kuwa tayari mchakato wa kuagiza mashine mbili za kisasa za Kuchinja na kuchakata nyama umekamilika ambapo Mashine itakuwa na uwezo wa  kuchinja, kusafisha na kuchakata Wanyama 2,000 kwa siku moja.

Katika hatua nyingine RC Makonda amefanya ziara ya kustukiza kwenye Mradi wa Ujenzi wa Soko la Kisasa la Kisutu na kumuagiza Mkandarasi wa ujenzi wa Soko hilo kufanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha ujenzi unakamilika na kukabidhiwa kabla ya mwezi May Mwakani.

Hatua hiyo imekuja baada ya RC Makonda kutoridhishwa kasi ya ujenzi wa soko hilo ambalo limekuwa likisuasua mara kwa Mara huku wataalamu wakitoa taarifa za wongo kuwa ujenzi unaenda vizuri.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages