Sunday, June 28, 2020

Home
KITAIFA
RC MAKONDA AKABIDHI KWA CHAMA CHA MAPINDUZI MIRADI ILIYOTEKELEZWA NA SERIKALI YA AWAMU YA TANO KWENYE JIMBO LA KAWE
RC MAKONDA AKABIDHI KWA CHAMA CHA MAPINDUZI MIRADI ILIYOTEKELEZWA NA SERIKALI YA AWAMU YA TANO KWENYE JIMBO LA KAWE
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo amefanya ziara kwenye Jimbo la Kawe kwa lengo la kukabidhi Miradi iliyotekelezwa na Serikali ya awamu ya tano kwa Chama cha Mapinduzi CCM ikiwa ni utekelezaji wa ahadi alizozitoa Rais Dkt. John Magufuli kupitia ilani ya Chama hicho.
Miongoni mwa miradi aliyokabidhi RC Makonda ni Mradi Mkubwa kabisa wa Kuchakata taka wenye thamani ya Bilioni 5.59 uliopo Mwabwepande, Mradi wa Shule Mpya ya sekondari ya Mabwe Tumaini Girls iliyogharimu Shilingi Bilioni 2.6 na Ujenzi wa Hospital ya Wilaya ya Kinondoni iliyopo Mabwepande yenye thamani ya Bilioni 2.4.
Aidha RC Makonda amekabidhi pia Mradi wa Matank makubwa matano na Pampu za kusambaza Maji zilizopo Changanyikeni, Ujenzi wa Kituo cha Afya Bunju chenye thamani ya milioni 600, Mradi wa Makazi ya Askari Mabwepande pamoja na kukabidhi Zahanati ya Mkoroshini kata ya Msasani yenye thamani ya Milioni 408.
Akizungumza katika ziara hiyo RC Makonda amewahimiza wananchi kuhakikisha wanachagua viongozi watakaowaletea maendeleo na sio viongozi wanaopinga kila jambo jema linalofanywa na serikali.
Hata hivyo RC Makonda amemuelekeza Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni kutafuta eneo kwaajili ya kujenga *Kituo cha Afya Kawe ili kusogeza huduma za Afya kwa wananchi wa kata hiyo.
Kesho RC Makonda ataendelea na ziara yake ya kukabidhi miradi kwa Chama cha Mapinduzi CCM kwa upande wa Jimbo la Kinondoni.
Tags
# KITAIFA
Share This
About Hassani Makero
Hassani Makero is a Wor'Out Media Country Manager located at Unguja-Zanzibar, Tanzania performing all technical issues concerning of Media Broadcasting activities, Satellites, and FM and Television equipments supplier.
Aside from that, Hassani Makero is also a Writer, Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 10 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs.
Aside from all above he own and operate his Blog known as Wor’Out Media since 2014.
Newer Article
Mbatia aitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuzingatia Haki
Older Article
KUTOKA MAGAZETINI JUNI 28, 2020
WATU 12,000 WAHOFIWA KUUGUA UGONJWA WA HIMOFILIA NCHINI
Hassani MakeroApr 19, 2025KILUPI: ATAKA KURA ZA MAONI ZISIWAGAWE WANACCM
Hassani MakeroApr 14, 2025Dkt.Dimwa - Akemea Rushwa Mchakato wa Kura za Maoni
Hassani MakeroApr 14, 2025
Labels:
KITAIFA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment