Thursday, July 30, 2020

HAKI MADINI yawajengea UWEZO wachekechaji MADINI
Ofisa miradi wa shirika lisilo la kiserikali la Haki Madini, Emmanuel Mbise akizungumza na wachekechaji wa madini ya Tanzanite wa Kata ya Naisinyai Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, kwenye mafunzo ya siku mbili ya elimu ya afya na usalama kwa wachekechaji.
Shirika lisilo la kiserikali la Haki Madini limewajengea uwezo wachekechaji 60 wa madini ya Tanzanite wa Kata ya Naisinyai Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara juu ya elimu ya afya na usalama.
Afisa miradi wa shirika la Haki Madini, Emmanuel Mbise akizungumza jana alisema wachekechaji hao watapatiwa mafunzo hayo kwa muda wa siku mbili.
Mbise alisema lengo la mafunzo hayo ni kuhakikisha wanachangia kupunguza athari za afya kwenye shughuli za uchekechaji.
Alisema pamoja na kutoa mafunzo hayo pia waliwapatia barakoa 400 kwa ajili ya kujikinga na vumbi wakati wakifanya shughuli zao za uchenjuaji mchanga wa madini ya Tanzanite.
"Pamoja na washiriki hao 60 pia kuna viongozi watano wakiwemo wa serikali hivyo kuwa na washiriki 65 ambao kwa namna moja au nyingine watakuwa mabalozi wazuri kwa wengine," alisema Mbise.
Mwenyekiti wa wachekechaji wanawake wa Naisinyai, Nairukoki Leiyan alisema mashirika mengine yaige mfano wa Haki Madini katika kuwajali wadau wa madini ya Tanzanite.
Leiyan alisema mafunzo hayo yatawasaidia kufanya shughuli zao ipasavyo na pia barakoa walizopatiwa zitawakinga na vumbi.
Mmoja kati ya wachekechaji hao Isaya Maliaki alisema mafunzo hayo yatawajengea uwezo zaidi wa kufanya kazi zao kwa usalama zaidi tofauti na awali.
Maliaki alisema pamoja na mafunzo hayo pia barakoa waliopatiwa zitawakinga na vumbi wakati wakifanya shughuli zao za uchenjuaji mchanga wa madini ya Tanzanite.
Alisema wachekechaji hao wakitekeleza namna walivyofundishwa watakuwa salama kwani watakuwa wanashika michanga kwa kutumia vikinga mikono wakati wakifanya kazi zao.
Afisa afya wa halmashauri ya wilaya ya Simanjiro Boniface Jacob aliwapongeza Haki Madini kwa kuwajengea uwezo wachekechaji hao wa madini ya Tanzanite.
Jacob alisema zaidi ya kuwapa mafunzo ya kuwezeshwa kujikinga na vumbi pia barakoa waliopatiwa zitawakinga na vumbi na maambukizi ya virusi vya corona kwani wanapaswa kuendelea kujikinga.
Tags
# BIASHARA
Share This
About Hassani Makero
Hassani Makero is a Wor'Out Media Country Manager located at Unguja-Zanzibar, Tanzania performing all technical issues concerning of Media Broadcasting activities, Satellites, and FM and Television equipments supplier.
Aside from that, Hassani Makero is also a Writer, Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 10 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs.
Aside from all above he own and operate his Blog known as Wor’Out Media since 2014.
Newer Article
Shibuda Apitishwa Kugombea Urais wa Tanzania 2020
Older Article
UWANJA WA MICHEZO TAIFA WABADILISHWA JINA SASA NI BENJAMIN WILLIAM MKAPA STADIUM
AKIBA COMMERCIAL BANK PLC YAPELEKA TABASABU KITUO CHA KULELEA WATOTO CHAKUWAMA
kilole mzeeMar 28, 2025Taasisi za Ulinzi wa Mlaji zimetakiwa kushirikiana na FCC
Hassani MakeroMar 21, 2025Safari ya Mafanikio ya NHC na Miaka Minne ya Mafanikio ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassani
Hassani MakeroMar 20, 2025
Labels:
BIASHARA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment