
SERIKALI kupitia Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk Leonard Akwilapo imeahidi kutoa sh milioni 200 kwaajili ya ujenzi wa madarasa matano katika Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), Kampasi ya Myunga ikiyoko Wilaya ya mkoani Songwe.
Ahadi hiyo ilitolewa jana na Dk Akwilapo alipofanya ziara ya kukagua ujenzi wa bwalo la chakula lililojengwa kwa fedha zilizotolewa na serikali kupitia wizara hiyo.
Ahadi hiyo ilikuja kufuatia ombi la wanafunzi la kuomba serikali kuboresha niundombinu ya kujifunzia ikiwa ni pamoja na madarasa, uwanja wa michezo na vifaa vya michezo pamoja na gari la kwaajili ya kwenda kwenye mafunzo viwandani.
Dk Akwilapo alisema anaamini kwa fedha hizo DIT itajenga madarasa mazuri yenye ubora unaofaa kwa kutumia wataalamu wa ndani wa Taasisi hiyo.
Akizungumzia ujenzi wa bwalo hilo, aliipongeza Taasisi hiyo kwa usimamizi mzuri wa rasilimali fedha uliofanikisha kukamilika ujenzi huo kwa asilimia 100.
Mkurugenzi wa Kampasi ya DIT Myunga, Dk Frank Lujaji alishukuru kwa msaada wa kijana Nozen kulipiwa ada ambapo alitoa wito pia kwa Taasisi nyingine kusaidia vijana wenye changamoto za kupata ada kwani wengi Wana uwezo wa kimasomo pamoja na nia ya kusoma.
No comments:
Post a Comment